Wananchi Mwanza walia na adha ya Ukosefu wa Stendi ya Igombe
Picha ikionyesha magari ya Abiria watokao Airpoti kwenda Usagara kupitia Buhongwa wakiwa wameegesha magari yao pembezoni mwa Barabara ya Kenyatta ili kushusha abiria baada ya Stendi ya Igombe iliyokuwa ikitumika kama Stand kumilikiwa na baraza kuu la waislamu mkoa wa Mwanza (BAKWATA).
Siku chache baada ya Baraza kuu la waislamu (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza kushinda kesi ya umiliki wa kiwanja namba 111 kitalu (T) Kilichopo barabara ya kenyatta eneo maarufu kama Stand ya Igombe kilichokuwa chini ya Halmashauri ya jiji la Mwanza baadhi ya wananchi jijini hapa wameibuka na kueleeza kero wanazopitia baada ya Baraza la waislamu kutwaa eneo hilo ambalo lilikua likitumika kama Stand ya kushusha abiria wanaotoka Airpot kwenda Buhongwa mpaka Usagara.
Global imefika eneo la Stand ya Igombe ambapo imekuta Stand hiyo ikiwa imefungwa huku magari yakiwa hayaruhusiwi kushusha abiria eneo hilo kutokana na umiliki wake kubadilika ambapo abiria sasa walikuwa wanatakiwa kushushwa kituo cha Tanesco kilichopo nje kidogo ya jiji la Mwanza jambo ambalo limeleta usumbufu kwa wananchi ambao walikusudia kushuka katikati ya mji ili kujipatia huduma za kijamii.
Mmoja wa wananchi aliyejitambulisha kwa jina na Petro Malulu amesema ” leo tumepata shida sana kushushwa katikati ya mjini kutokana na eneo la Stand ya Igombe kufungwa , maana sisi abiriia tuliokua tunatoka Aipot kutumia magari yanayokwenda Usagara kupitia Buhongwa tulikosa pa kushukia baada ya eneo tulilozoea kufungwa tunaiomba serikali itutengee eneo jingine kwaajili ya matumizi ya Stand ya magari madogo ili kuondoa usumbufu ambao umejitokeza leo” alisema
Picha ikionyesha Kiwanja nambari 111 kilichokuwa kikitumika kama Stand ya Igombe ikiwa imefungwa kuruhusu Ibaada maalumu ya Bakwata kufanyika iliyokuwa na lengo la kumshukuru Mungu kwa baraza hilo kushinda keshi hiyo nambari 58 ya mwaka 2017 iliyokua na shauri nambari 150 ya mwaka 2020 ambapo wananchi leo wamekumbana na kadhia ya kutoshushwa eneo hilo kutkana na magari kutoruhusiwa kusimama.