Na Denis Mtima/GPL
WIZARA ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini imewaomba wananchi kutembelea vituo vya hali ya hewa ili kuona shughuli zinazotolewazo na mamlaka hiyo na kujifunza.
Hayo yamesema leo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Dk. Agnes Kijazi, wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam kuadhimisha siku ya kuanzishwa kwa Shirika la Hali ya Hewa Duniani ambalo lina wanachama 191.
Kijazi alisema mamlaka kwa upande wake hutembelea na kutoa elimu kwa vijana wa baadhi ya shule na vyuo mbalimbali nchini kupitia ofisi zake zilizopo nchi nzima.
Kaulimbiu ya siku ya maadhimisho hayo ni: ”Tuyaelewe mawingu na umuhimu wake”.
Comments are closed.