Wananchi Wazidi Kuneemeshwa Na Kampeni Ya Serengeti Lite, Maokoto Ndani ya Kizibo Wanywaji Wajizolea Laki Tanotano

Dar es Salaam, 4 Novemba 2023: Kampeni ya Maokoto Ndani ya Kizibo inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia bia yake ya Serengeti Lite imezidi kuwanufaisha wananchi wanaotumia bia hiyo na kujishindia maokoto ndani ya kizibo cha bia hiyo.
Mkazi wa Mbezi jijini Dar, David Swai jana Jumamosi alikuwa ni miongoni mwa washindi waliokabidhiwa shilingi laki tano baada ya kununua bia ya Serengeti Lite kwenye moja iliyopo Mbezi Mwisho jijini na kukumbana na Okoto la shilingi laki tano ndani ya kizibo hicho.

Akiongea kwa furaha kwenye hafla ya kumkabidhi okoto hilo iliyofanyika jana kwenye Baa ya TTG iliyopo, Kimara Korogwe jijini, Swai alisema akiwa kwenye baa hiyo kuna mtu alimshauri kutumia bia hiyo ambayo kwasasa ipo kwenye kampeni Maokoto Ndani ya Kizibo na alipojaribu kama masihara alijikuta akiondoka na ushindi huo.
Mshindi huyo alisema okoto hilo linamsaidia kuongezea pale palipopungua kwenye bajeti zake.
“Pesa haikosagi matumizi na hakuna mwenye pesa zikamtosha hivyo nami okoto hili litanisaidia kuongezea pale palipopungua”. Alisema mshindi huyo.
Mshindi huyo alikabidhiwa okoto lake na Afisa Msimamizi wa Bia za Serengeti Kanda ya Kimara mpaka Mbezi, Hillary Moshi.
Sambamba na mshindi huyo washindi wengine wa Maokoto ndani ya Kizibo nao walikabidhiwa maokoto yao maeneo mbalimbali.