The House of Favourite Newspapers

Wanandoa Wadai Fidia Mil 376 Baada ya Kanisa Kuifuta

0

MUHWEZI BENSON na Akankwasa Sophie wamedai fidia ya Tsh milioni 376 kwa kanisa la ‘Church of Uganda’ baada ya kufuta ndoa yao iliyogharimu takribani milioni 471 kuiandaa.

 

Mwanasheria wa wanandoa hao alisema kuwa wateja wake wamekuwa na hali ngumu hivi sasa kisaikolojia na wameingia madeni makubwa ya kitu ambacho hakijafanyika, pia waliotoa michango wamekuwa wakiwaita wezi, jambo ambalo linawaumiza zaidi.

 

Walipewa ujumbe wa kuwa ndoa yao haitafungwa ndani ya masaa 48 kabla ya ndoa, hiyo ni baada ya Sarah Kemigisha kudai kuwa yeye ni mke wa Muhwezi tangu 2001.

 

Muhwezi amesema alifuata hatua zote za kufunga ndoa na alibadili dini na akabatizwa. Na wazee wa kanisa walimwambia anaweza kufunga ndoa kwa kuwa ndoa yake na Sarah haikutambulika na kanisa.

 

Muhwezi na Sophie wamekuwa kwenye mapenzi tangu 2014 na wana watoto wawili. Kanisa limesema lina uwezo wa kuacha kufungisha ndoa hata kanisani kwenyewe siku ya ndoa.

 

Leave A Reply