The House of Favourite Newspapers

Wanandoa Waliodumu Zaidi Waingia Rekodi za Guinness

0

JULIO MORA (110) na Waldramina Quinteros (104)  wenza walioana mwaka 1941, kwa ndoa ya siri baada ya familia zao kutoidhinisha mahusiano yao. Ndoa yao, iliyoanza kwa siri imedumu kwa miaka 79 na wenza hawa kwa pamoja wameishi zaidi ya miaka 215 kwa ujumla.

Julio na Waldramina wamekuwa pamoja kwa muda mrefu kuliko wenza wengine wengi walio hai. Wawili hawa wametambulika kuweka rekodi ya dunia ya Guinness kwa wenza walio na umri mrefu zaidi duniani.

 

Wapenzi hao raia wa Ecuador, kwa upande wao, Mora alizaliwa tarehe 10 mwezi Machi, mwaka 1910 na Bibi Quinteros tarehe 16 mwezi Oktoba mwaka 1915. Kuna ndoa zenye umri mrefu ambazo Guinness inazitambua, lakini hakuna yenye wenza walio na umri mkubwa zaidi.

Wapenzi hawa walioana mwaka 1942 katika kanisa la kwanza kujengwa mjini Quito, Uhispania: La Iglesia de El Belen. Julio aliwakimbia wazazi wake na kwenda kumuoa mpenzi wake baada ya kutopata ridhaa ya familia. ”Hatukuachana,” alisema Bi Quinteros.

 

Wote ni walimu ambao wamestaafu na wanaishi eneo katikati ya mji wa Quito, mji mkuu wa Ecuador. Kwa pamoja wanaweza kukusanya watu wengi kutokana na uzao wao: wana watoto wanne walio hai, wajukuu 11, vitukuu 21 na kilembwe kimoja.

Mwanzoni mwa mwaka, mmoja wa wajukuu wao alisema kuwa wazee hao huenda wakawa miongoni mwa wenza walio na umri mkubwa duniani. Mtoto wao Cecilia kisha alituma nyaraka kwa Guinness kisha wakapata uthibitisho katikati ya mwezi Agosti.

 

Wote wako timamu na wenye afya njema, Cecilia anesema, ingawa afya yao ya akili ilitikiswa kutokana na janga la corona. ”Kwa mwezi mmoja wamekuwa tofauti, wamekuwa wenye huzuni, kwa kuwa wanakosa mikusanyiko ya familia,” alisema.

Alipoulizwa kama ana ushauri kwa wale wanaotamani kuishi maisha marefu, Bi Quinteros amesema: ”Ninashauri kusema kweli. Usiseme uongo, uongo unaweza kuipoteza dunia.”

Awali waliokuwa wanashikilia rekodi ya kuwa wenza wenye umri mrefu walikuwa wakazi wa Texas Charlotte na John Henderson, ambao kwa pamoja walikuwa na jumla ya miaka 212 na siku 52.

 

Leave A Reply