The House of Favourite Newspapers

Wanaodaiwa Kufanya ‘Biashara ya Walemavu’ Wafikishwa Mahakamani

0

WASHITAKIWA 15 wanaodaiwa kuwatumikisha walewavu waliokamatwa katika maeneo ya Tandale jijini Dar es Salaam hivi karibuni, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 41 ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu na kuwatumiskisha kama ombaomba mtaani na kujiingizia kipato kinyume cha sheria.

 

Akisoma hati ya mashtaka wakili wa serikali, Mkunde Mshanga na wakili wa serikali Mkuu, Wankyo Simon, amesema washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Agosti 2020 na Januari Mosi 2021 katika maeneo ya Tandale Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa makosa hayo 41 yanayowakabili washtakiwa 15 inadaiwa mshtakiwa Sadikieli Zebedayo na Yusufu Mohammed akiwa na wengine waliwatumikisha walemavu kinyume cha sheria kwa kuwafanya ombaomba mtaani na kujiingizia kipato kupitia shughuli hiyo, kinyume cha sheria ya Usafirishaji Haramu wa Binadamu.

 

Katika kosa la mwisho linalomkabili mtuhumiwa, Sadikieli Zebedayo ambaye ni wa kwanza, inadaiwa alikwepa kulipa kodi kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya zaidi ya Sh. mil. 31 kinyume cha sheria ya uhujumu uchumi.

 

Baada ya kusomewa mashtaka yanayowakabili,  hakimu aliyesikiliza kesi hiyo, Kassian Matembele, amesema kuwa kesi hiyo haina dhamana kwa kuwa ni ya uhujumu uchumi na hivyo washtakiwa watapelekwa gerezani hadi itakapotajwa tena Januari 26, 2021.

 

Oparesheni ya kusaka wanaojinufaisha na watu wenye ulemavu kupitia kuombaomba ilianza rasmi Januari Mosi, mwaka huu ambapo Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia wenye ulemavu, Ummy Nderiananga,  kwa ziara maalum iliyofanyika usiku na kubaini biashara hiyo ambayo imekuwepo kwa miaka mingi.

Leave A Reply