The House of Favourite Newspapers

Wanaodaiwa Kumteka Tarimo Hawa Hapa, Wakana Shtaka Lao

0

Watuhumiwa 6 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kivukoni iliyoko Kinondoni Jijini Dar es Salaam na kusomewa shtaka moja la jaribio la kumteka Mfanyabiashara Deogratius Tarimo.

Akiwasomea shtaka hilo Wakili wa Serikali John Mwakifuna mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Ramadhan Rugemalila.

Washtakiwa hao sita ni Bato Bahati Tweve, Nelson Elmusa, Anitha Alfred Temba, Isaack Mwaifuani, Fredrick Juma Msatu, Benki Daniel Mwakalebela wote wakazi wa Dar

Inadaiwa Novermber 11, 2024 eneo la Kiluvya Madukani Washtakiwa wote sita wanadaiwa kumteka Deogratius Tarimo kinyume cha sheria ambapo wote kwa pamoja wamekana shtaka hilo huku Hakimu akiweka wazi kuwa dhamana yao iko wazi.

Hakimu Rugemalila amewataka washtakiwa hao kutimiza masharti ya dhamana ya kila mmoja kusaini bondi ya Shilingi Milioni 10 kila mmoja na kuwa na wadhamini wawili wenye barua ya utambulisho na kitambulisho cha NIDA na kutotakiwa kutoka nje ya DSM bila ruhusa ya Mahakama.

Washatkiwa wote sita wameshindwa kukamilisha masharti ya dhamana wamepelekwa rumande hadi Drcember 19, 2024 ambapo kesi inakuja kwa ajili ya maelezo ya awali na usikilizwaji na upelelezi wa kesi hiyo umekamilika

Leave A Reply