The House of Favourite Newspapers

Wanaokwenda kupewa ofa baa utawajua tu!

0

WANAPOONGOZANA watu kadhaa kwenda baa kunywa pombe au vinywaji vingine, mwenye pesa utamjua tu na wanaopelekwa kupewa ofa pia utawajua!

Mara nyingi, ikitokea wakaenda baa kwa kutumia gari moja, wakishashuka, mwenye pesa ndiye anayeachwa atangulie mbele.
Mfano, baada ya kushuka kwenye gari halafu mwenye pesa akachelewa kushuka, wao huwa hawataki kutangulia kuingia baa mpaka ‘tajiri’ ashuke kwanza.
Utawaona wanatembea huku na kule wakijifanya wanaongea na simu na watu wao mbalimbali ili tu dakika ziende mbele, mwenye pesa ashuke.
Wakishafika baa sasa, wanaopelekwa kupewa ofa wao huwa hawana ubavu wa kuchagua pa kukaa. Tajiri ndiye anayeamua, akishafika kwenye meza na kuvuta kiti na wao ndiyo utawaona wanakaa.
Moyoni huomba Mungu wahudumu waanze kumuuliza tajiri ili na wao wapate mwanga wa kinywaji gani aagize. Tajiri akisema bia na wao bia, akisema maji, na wao maji mpaka tajiri awabadilishie kwa kuwaambia; ‘nyiee, si mnakunywa bia!”

Leave A Reply