The House of Favourite Newspapers

Wanaosumbuliwa na mba, tiba hii hapa!

0

Kwenye makala zilizopita nimewahi kuandika urembo unaohusu kutibu mba wa kichwani kwa kutumia uwatu, limao nk.

Kutokana na wasomaji kuendelea kuomba ushauri wa kinachoondoa mba kichwani, wiki hii nimeamua kuwaletea tiba nyingine ambayo ni siki ya tufaha ‘apple’.

Ni tiba nzuri inayoweza kukupa matokeo kwa haraka, mbali na kuponya mba pia inajaza nywele.

Jinsi ya kutumia

Chukua maji kiasi na siki inayolingana na maji hayo, tikisa kidogo mpaka ichanganyike.

Baada ya hapo osha nywele zako zitakate kisha chukua siki uliyoiandaa ambayo tayari imeshachanganywa, paka chini kwenye ngozi pale shina la nywele linapotokea.

Baada ya kupaka acha kwa saa moja au mawili, kisha osha ukaushe na baadaye paka mafuta unayotumia kwenye nywele.

Pia kwa kuifanya ijaze nywele sana unaweza kuchanganya na mafuta ya chai (Tea tree oil) ambapo utaweka matone 15 au 20 kwenye ule mchanganyiko wako, mafuta haya wengi wamekuwa wakiyakosa ila kama unayo ni bora zaidi kuyachanganya.

Hata hivyo, chunguza mafuta unayotumia kwanza kabla ya kupaka kwani mengine yanasababisha mba.

Leave A Reply