The House of Favourite Newspapers

Zifahamu Athari za Kunywa Pombe Kupindukia!

UNYWAJI wa pombe kupitia kiasi si mzuri kwa afya yako, kitu kilichothibitishwa kisayansi miaka kadhaa iliopita. Katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni, utafiti umeonyesha kuwa imani za zamani kwamba glasi moja ya mvinyo wakati wa chakula ni muhimu ni potofu.

Hivi sasa athari za unywaji wa pombe zinazidi kujulikana. Kundi moja la wanasayansi kutoka chuo kikuu cha Rutgers nchini Marekani  na watafiti kutoka chuo cha Yale nchini humo, wamegundua kwamba unywaji wa pombe unaweza kuathiri chembechembe  za vinasaba vya binadamu (DNA) na kumfanya atamani kunywa pombe zaidi.

Watu wengi pia wanahoji iwapo kinywaji kimoja kina athari mbaya kwa afya. Ili kupata jibu, kundi hilo la watafiti liliamua kuangazia uchanganuzi wake katika jeni mbili zinazohusiana na kudhibiti tabia wakati tunapokuwa chini ya shinikizo la pombe.

Moja ni ile ya PER2 inayoshawishi maisha ya miili yetu na nyingine ya POMC, ambayo inadhibiti utaratibu wetu wa kukabiliana na dhiki.

 

Wakilinganisha wanywaji wa kadiri na wale wanaokunywa pombe kwa wingi, wanasayansi wamegundua kwamba jeni za watu wanaokunywa pombe kwa wingi hubadilika.

Kwa wale wanaokunywa kwa wingi, jeni zao hutoa protini polepole na hupata hamu ya kunywa wakati wanapokumbwa na matatizo

Mabadiliko ya jeni huongezeka kutokana na vinywaji zaidi. Unapokunywa pombe zaidi unazidi kuharibu jeni,  hatua inayotufanya kuwa na hamu ya kunywa pombe zaidi na zaidi.

“Tumegudua kwamba watu wanaokunywa pombe nyingi wanabadilisha chembechembe zao za DNA katika njia inayowafanya kutaka kunywa zaidi,” alisema Profesa Dipak K Sarkar, mwanzilishi wa utafiti huo unoaoongozwa na chuo kikuu cha Rutgers.

“Hii inaweza kusaidia kuthibitisha kwa nini pombe ina mvuto mkubwa”, aliongezea

Watafiti wanatumai kwamba ugunduzi wao utawaruhusu kutambua viashiria vinavyoweza kupimwa kama vile protini au jeni zilizobadilishwa kutabiri hatari ya mtu anayekuwa na unywaji wa kiwango cha juu jinsi atavyolindwa asiweze kunywa zaidi.

 

Comments are closed.