Wanasayansi Watabiri Corona Itaisha Uingereza Septemba

WANASAYANSI wametabiri kwamba virusi vya corona, vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19, vitakuwa vimetoweka nchini humo mezi Septemba mwaka huu.
Watafiti nchini Singapore wametumia njia za utaalam wa kiwango cha juu kutambua kipindi halisi ambacho janga hilo litakuwa limetoweka duniani kote, ambapo imeonyesha kwamba virusi hao wenye maangamizi makubwa watakuwa hawako tana nchini Uingereza ifikapo Septemba 30 mwaka huu, linasema gazeti la Daily Stars.
Hali hiyo inaiweka Uingereza mbele ya Marekani ambayo inasemekana itaondokana na virusi hivyo Novemba 11 mwaka huu.
Hata hivyo, Italia na Singapore zitaondokana na ugonjwa huo kwanza ambapo inatarajiwa kupungua ifikapo Agosti 12 na Julai 19 kwa mfuatano.
Wakati huohuo, profesa maarufu wa Chuo Kikuu cha Oxford ametabiri kwamba viwango vya vifo nchini Uingereza vitatoweka ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.
Hivi sasa Uingereza inashika nafasi ya nne duniani miongoni mwa nchi zilizokumbwa na ugonjwa huo. Hata hivyo, Chuo Kikuu cha Singapore kimesema utabiri huo si “wa uhakika”na kwamba unaweza kubadilika wakati wowote.

