The House of Favourite Newspapers

Wanasiasa, Wanataaluma Washiriki Mdahalo Kuhusu Demokrasia

0
John Shibuda wa Baraza la Vyama vya Siasa akizungumza katika mjadala huo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Twaweza, Aidan Eyakuze, Akizungumza kwenye hafla hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea.
..Zitto Kabwe akichangia katika mdahalo huo.

TAASISI ya Twaweza ikishirikisha wadau mbalimbali,  leo imefanya mdahalo kutathmini hali na mustakabali wa demokrasia nchini  ambapo wadau, wanasiasa na watu mbalimbali wameshiriki.

 

Mdahalo huo umefanyika katika viwanja vya Karimjee jijini  Dar es Salaam leo ambao ulianza majira ya saa tatu  asubuhi hadi saa kumi jioni.

 

Katika mazungumzo hayo, palikuwa na uwasilishaji wa takwimu za kidemokrasia, mjadala huru, maigizo na maonyesho ya sanaa za kidemokrasia.

 

Mwongozaji wa mdhalo huo alikuwa ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Twaweza ambapo miongoni mwa watu wengine walikuwa ni mmilili wa mtandao wa Jamii Forum, Maxence Melo;  Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe; na   John Shibuda wa Baraza la Vyama vya Siasa.

 

NA DENIS MTIMA/GPL

Matukio kama haya na mengine, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

VIDEO: DK SHIKA KUWEKA HISTORIA USIKU WA 900 ITAPENDEZA

Leave A Reply