Wanaume Walio Uchi Wanapoisaka ‘Fimbo Ya Bahati’! (PICHA)

 

MAELFU ya wanaume waliokuwa nusu uchi na waliovalia vinguo vyeupe vinavyoanzia kiunoni, venye kuficha tupu zao kwa mbele na kuyaacha makalio wazi, hivi karibuni walishiriki tamasha maalum la kutafuta fimbo zilikuwa zimerushwa katika umati wa watu.

Wale waliopata fimbo zenye urefu wa sentimita 20, ambazo zinaitwa “shingi”, wanaaminika kuwa ndiyo wanaume wenye bahati zaidi mwaka huu (2019).

 

 

Maadhimisho haya yalikuwa ya 510 katika historia ya Japan ambapo maelfu ya washiriki  huoga maji ya baridi katika mto Yoshii ili  kutakaswa kabla hawajaanza kutafuta fimbo ya bahati.  Mara baada ya kumaliza kuoga maji hayo baridi, taa huwasha.

 

 

Mkuu wa sehemu hiyo ya kuabudia husimama juu katika jukwaa la mita nne na kurusha fimbo hizo mbili katika mkusanyiko mkubwa wa watu. Watu wawili watakaoweza kuzipata fimbo hizo hutajwa kuwa washindi wenye bahati.

 

 

Tamasha la ‘Saidaiji-eye’ ni miongoni mwa matamasha makubwa katika tamaduni za Japan katika kalenda ya mwaka. Vilevile tamasha hili linafikiriwa kuwa linaleta mazao mazuri katika mwaka.

Loading...

Toa comment