Wanawake Brazil Kulipwa Sawa na Neymar
WACHEZAJI wa timu ya taifa ya wanawake ya Brazil watalipwa mishahara sawa na wachezaji wa timu ya wanaume, ametangaza Rais wa Shirikisho la Boka Brazil (CBF), Rogerio Caboclo.
CBF inakuwa miongoni mwa mashirikisho machache duniani yanayolipa posho sawa kwa timu za taifa za wanawake na wanaume, mataifa mengine yanayofanya hivyo ni Australia, Norway na New Zealand.
Malipo haya yataanza katika michuano ya Olympiki itakayofanyika mwakani na katika fainali za Kombe la Dunia.
Amesema, “Itakuwa sawa kwa wote kama mapendekezo ya FIFA yanavyotaka kwenye soka la wanawake, hivyo hakutakuwa na utofauti wa jinsia.”