Wanawake Kupewa Talaka Kupitia Ujumbe wa Simu

 

SHERIA mpya nchini Saudia inawalinda wanawake kutopewa talaka bila kujua, lakini kuanzia siku ya Jumapili hii, mahakama zitatakiwa kuwaelezea wanawake kupitia njia ya ujumbe wa simu kwamba wamepewa talaka.

 

Mawakili wanawake wanapendekeza kuwa hatua hiyo itamaliza kile kinachotajwa kuwa talaka za siri – ambapo wanaume hutoa talaka bila kuwaelezea wake zao.

 

Amri hiyo itahakikisha kuwa wanawake wanajua hali ya ndoa yao na itawalinda dhidi ya mgawanyo wa mali zilizotokana na ndoa hizo (masurufu).

 

Mwaka uliopita marufuku ya wanawake kuendesha magari iliondolewa na mahakama nchini Saudia.

 

Hata hivyo, wanawake bado wako chini ya usimamizi wa wanaume.

 

”Sheria hiyo mpya itahakikisha kuwa wanawake wanapewa haki zao za masurufu wakati wanapopewa talaka,” alisema wakili Nisreen al-Ghamdi.

 

Pia inahakikisha kuwa uwezo wowote utakaotolewa na mahakama hautumiki vibaya.

 

”Wanawake wengi wamewasilisha malalamiko yao katika mahakama za rufaa kwa kupewa talaka bila ya wao kujua,”  kulingana na wakili Samia al-Hindi.

 

Hatua hiyo mpya inasemekana kuwa miongoni mwa mabadiliko ya kiuchumi na kijamii yalioshinikizwa na Mwanamfalme Mohammed bin Salman, ikiwemo kuwaruhusu wanawake kuingia uwanjani na kutazama mechi za kandanada mbali na kufanya kazi ambazo awali zimekuwa zikifanywa na wanaume pekee.

 

Kuna vitu vingi ambavyo wanawake wa Saudia bado hawaruhusiwi kufanya bila ya kuomba ruhusa kutoka kwa wasimamizi wao wa kiume kama vile waume zao , baba zao,  ndugu wa kiume ama watoto wao.

 

Vitu hivyo ni:

 

  • Kuwasilisha maombi ya pasipoti.

 

  • Kusafiri katika mataifa y kigeni.

 

  • Kuolewa

 

  • Kufungua akaunti ya benki.

 

  • Kuanzisha biashara

 

  • Kuondoka jela

 

Hali hiyo ya kusimamiwa na wanaume imesababisha taifa hilo kuwa miongoni mwa mataifa ambayo usawa wa kijinsia umekandamizwa eneo hilo la Mashariki ya Kati.

Loading...

Toa comment