The House of Favourite Newspapers

Wanawake Wafanyabiashara Kariakoo Wawezeshwa na Tigo Namna ya Matumizi ya Fedha Kidijitali  

0
Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Pesha (katikati) akizungumza kwenye mkutano huo.

Kampuni ya mawasiliano ya Tigo nchini imesema itaendelea kuunga mkono juhudi za serikali za kuhakikisha inachangia ujumuishwaji wa kifedha kwa wananchi kupitia huduma zake za kifedha kwa njia ya kidijitali.

Hayo yameelezwa na Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Pesha jijini Dar es salaam wakati wa kikao kilichowakutanisha Tigo na wafanyabiashara wanawake wa Kariakoo ikiwa ni mkakati mkubwa wa tigo kuhakikisha wanaunga mkono wanawake kukua kibiashara kupitia huduma za tigo.

Wadau wakisikiliza kiumakini yanayoendelea.

Angelica amefafanua kuwa Juhudi hizi ni moja ya mkakati wa kuunga mkono serikali ya kuhakikisha wanafikia makundi mbalimbali ikiwemo wanawake lakini pia kufikia uchumi jumuishi,hivyo tigo imetenga muda wake kuweza kuwasikiliza na kuona ni suluhisho zipi wanazoweza kutoa katika huduma zake kwa ajili ya biashara ambayo itakua na tija kwa mfanyabiashara hasa za kidigitali.

Aidha ameongeza kuwa mkutano huo unawasaidia wao  kama tigo kuwasikiliza na kuona ni changamoto gani ambazo zikifanyiwa kazi zitaleta suluhisho lakini pia mpango mkakati wa muda mfupi na mrefu kuhakikisha wanawake wanawezeshwa kufanya biashara kwa urahisi,usalama,na kupitia tigo pesa ili kuharakisha matarajio ya kufikia uchumi wa kidigitali.

Akizungumza kwa niaba ya wanawake wafanyabiashara wanawake Fransiska Limo amesema kuwa tigo wamekuja kufungua mawazo yao,wamepata elimu ya uelewa wa namna ya kutunza kumbukumbu za fedha na  mahesabu,lakini pia watatumia mtandao wa tigo katika kufanya miamala kidigital hasa kupitia lipa namba na huduma zingine zinazomfanya mfanyabiashara afanye malipo bila kuwa na pesa taslim.

Kampuni ya mawasiliano ya tigo imekutana na Zaidi ya wanawake wafanyabiashara 35  kutoka eneo la biashara kariakoo lakini pia huo ni mwanzo tu,matarajio yao ni kukutana na wafanyabiashara wote nchini ili kusaidia kuleta ujumuishwaji wa kifedha kwa watanzania wote.

Leave A Reply