The House of Favourite Newspapers

Ni Kweli Wanawake Wazuri Hawaoleki? Soma Hapa

0

TUNAFAHAMUkwamba hakuna mwanamke mbaya. Ila katika mazingira ya kawaida wapo ambao wanakuwa na umbo fulani la kuvutia zaidi. Wanawake ambao wana mwonekano wa kuwa kama vile pambo.

Kwa kawaida, wanawake wa aina hii huwa wanakuwa na kasumba zao. Ule uzuri huwa unawazuzua kidogo akili kutokana na vile ambavyo anaona kila mwanaume anayekutana naye anamuwewesekea.

Anapata jeuri ya kuona kwamba yeye ni mzuri.Hapo ndipo kichwa kinapovimba.

Anapata kiburi kwamba hawezi kubabaishwa na mwanaume. Akiachwa leo kesho tu atapata mwanaume mwingine. Na huyo mwingine naye akizingua, atapata mwingine haraka tu.

Mtindo wa maisha yake si wa kutulia na mwanaume mmoja. Anafahamu soko lake ni kubwa hivyo ni ngumu sana kuwa na hofu ya kukosa mwanaume.

Anajikuta yeye ni mtu wa wanaume tofautitofauti, kutulia na mmoja hawezi.Ndugu zangu, aina hii ya maisha ilivyozoeleka ndiyo imezua kasumba kwamba mwanamke mzuri huwezi kumuoa.

Wanaume wengi wamejazana maneno kwamba, wanawake wa aina hii ni viburudisho. Wanawake wa kuoa wapo lakini si wao.Mtu anakuwa na mkewe nyumbani wa kawaida sana lakini nje anakuwa kiburudisho cha aina hiyo ili kusuuza moyo wake. Nyumbani anaye wa kuishi, kuzaa naye watoto.

Kiburudisho kinatumika kwa wakati tu anapokuwa anataka kuburudika.

Mathalan anataka kutoka kwenda viwanja vya starehe, kwenda mahali ambapo ataonekana ana demu mzuri ambaye wengine pia watamzea mate.

Atamtumia kwa siku hiyo halafu mwisho wa siku anamuacha, anarudi kwa mkewe.Lakini hapa tutafakari pamoja, ni kweli kwamba wanawake wazuri hawafai kuolewa?

Kwamba ni kweli wanaume wote wana mawazo hayo? Je, ni kweli wanawake hawa wazuri nao wameridhika na kasumba hiyo kwamba wao ni wa kutumika tu?Watatumika na wanaume hadi lini? Mustakabali wa maisha yao utakuwa ni nini hapo baadaye.

Hii sio sawa, hili suala huletwa na akili ya mwanamke mwenyewe.

 

Mifano ipo mingi tu. Wapo wanawake wazuri ambao wameolewa na ndoa zao hazina vurugu zozote.

Walifanikiwa kivipi? Kujitambua. Walijua thamani yao. Mwanamke si chombo cha kujistarehesha, mwanamke anapaswa kuheshimika. Kumbe pamoja na uzuri, hehima ya yake ni kitu cha msingi sana.

Wewe kama ni mzuri, huna sababu ya kuutumia uzuri huo vibaya.Ukifanya hivyo ni tabia yako mwenyewe na ni maamuzi yako binafsi.

Unaleta tu sura mbaya kwa wanawake wa aina yako lakini si kwamba wote ndio wapo hivyo. Wapo wanawake ni wazuri lakini wanajiheshimu, wanavaa vizuri na wanaishi kwenye ndoa miaka nenda rudi.

Achana na kasumba ya kwamba mwanamke mzuri hafai kuolewa, anafa sana. Kikubwa ni akili ya mwanamke mwenyewe. Akichagua kuwa chombo cha kutumika ni yeye, akiamua kutulizana pia inawezekana tu.

Anayejitambua atajiheshimu, ataitafuta thamani ya mwanamke kuolewa. Atajitunza, atavaa mavazi ya kujisitiri. Kichwa chake hakitachetuka kwa kuona anatongozwa sana.

Zaidi atamchagua mmoja mwaminifu na mwenyew mapenzi ya kweli basi atafanya naye maisha.Natumaini mtakuwa mmenielewa, tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri

 

Leave A Reply