The House of Favourite Newspapers

Wanazeeka na Bongo Fleva Yao

2
Khaleed Mohamed ‘TID’

 

HIVI karibuni kwenye Ukumbi wa Next Door, Msasani jijini Dar, nilimshuhudia msanii mkongwe kwenye Muziki wa Bongo Fleva, Khaleed Mohamed ‘TID’ akifanya makamuzi ya hatari kiasi cha kujikusanyia kijiji chake katika onesho maalumu lililoandaliwa na msanii mwenziye, Ruta Bushoke.

 

Ruta Bushoke

 

Uwezo aliouonesha TID ‘Mnyama’ ulikuwa ni wa kipekee sana. Ni kweli jamaa anajulikana kuwa na uwezo mkubwa wa kuimba na kucheza pamoja na mashabiki wake jukwaani, lakini siku hiyo ni kama alizidi-sha.

Q Chillah

 

TID ambaye nimem-fuatilia tangu enzi za wimbo wake wa Girlfriend na kwenye matamasha mbalimbali, siku hiyo nilimuangalia katika jicho la tofauti na kufahamu ingawa umri wake unakata na ametoka mbali na muziki huu, bado ana nguvu na ari ya kukimbizana na vijana wapya ambao wapo kwenye gemu kwa sasa! Ana uwezo mzuri wa kuimba ‘live’ pamoja na kucheza vizuri.

Chegge na Temba

 

Nilichokiona kwa TID ndicho ninachokiona kwa baadhi ya wasanii wakongwe, walioanza Bongo Fleva tangu miaka ya mwan-zoni mwa 2000 ambao bado muziki huo ni ajira inayowapa mkwanja wa kuendesha maisha yao ya kila siku.

 

Mr Blue

 

Wasanii hao ni pamoja na TID, Mr Blue, Q Chillah, Chegge, Temba, Fid Q, Dully Sykes, Madee na wengine kibao. Hawa ni baadhi ya wasani wanaozeeka na Bongo Fleva yao na ukiwazungumzia mmojammoja na kazi zao za sasa utakubaliana nami kuwa bado wana uwezo mzuri na wanawakalisha wasanii vijana walio katika gemu kwa sasa.

 

Jay Moe

Lakini pia ukiangalia kwa miaka hiyo ya mwanzoni mwa 2000, kulikuwa na ushindani kwa wakali wa Hip Hop kama Solo Thang, Afande Sele, Soggy Doggy, Inspector Haroun, Jay Moe, Mchizi Mox na wengine wengi ambapo kwa sasa ni kama gemu la muziki huo limepoa.

Kwa sasa ukimzungumzia mkali kama Madee na kumlinganisha na wasanii kama Stamina, Izzo Bizness, Stereo na wengineo, utaona kwamba jamaa bado anazeeka na Bongo Fleva yake.

Madee

 

Ukitaka kujua anawakalisha vipi unaweza kutazama mafanikio ya nyimbo zao kwenye mitandao, kwa mfano Wimbo wa Hela wa Madee umetazamwa na zaidi ya watu 158, 674, wakati wimbo wa Izzo Buzness uitwao Tumeoana ambao pia hauna muda mrefu umeangaliwa na watu 125,018. Lakini ukitazama ngoma ya Stamina aliyomshirikisha Maua Sama, iitwayo Love Me umeangaliwa na watu wasiofika hata 2000.

 

 

Sasa huyo ni Madee tu na hapo hujawa-zungumzia wakali kama Fid Q ambaye hakuna asiyejua habari yake kila anapoachia ngoma. Bado Dully Sykes, Q Chillah ambaye ameung’arisha wimbo mpya wa Chid Benz uitwao Muda, Mr Blue, ama Chegge na Temba ambao kila wanapotoa ngoma zinafanya vizuri kwenye media mbalimbali na chati za burudani.

Saida Karoli

 

Ukweli ni kwamba wanam-uziki hawa wana-hitaji heshima kwa mch-ango walio-utoa na wanaoe-ndelea kuutoa kwenye gemu ya muziki maana wamekua nao na wanazeeka nao!

Wasanii wengi walianza nao pamoja ama ‘walihit’ nao wakiwemo, Afande Sele, Bwana Misosi, Ferooz, Daz Baba na wengine wengi lakini kwa sasa hawasikiki tena ama hata wakijaribu kufurukuta bado ngoma zao zinagonga mwamba!

 

BONIPHACE NGUMIJE | IJUMAA WIKENDA

 

Full Event: Miaka 15 ya Saida Karoli Kwenye Game ya Muziki

2 Comments
  1. […] mwa marapa wa kike wanaofanya vizuri kwenye gemu ya Bongo Fleva, Chemical ni miongoni mwao ambapo hivi karibuni ameonekana kwenye muonekano mpya wa […]

  2. […] na aliyekuwa mke wake ambaye pia ni mzazi mwenziye, zinaendelea kuutesa ubongo wa mwanamuziki wa Bongo fleva, Nuh Mziwanda, ambapo hivi karibuni ameamua kuomba ushauri kwa mashabiki wake, juu ya mwanamke gani […]

Leave A Reply