The House of Favourite Newspapers

Wanne Mahakamani Wakijaribu Kulipua Shamba la Mugabe

0

Robert-Mugabe_2137784bRais wa Zimbabwe, Robert Mugabe.

WANAUME wanne, wakiwemo askari wawili wa jeshi la ulinzi, wamefikishwa mahakamani nchini Zimbabwe wakikabiliwa na shitaka la kula njama za kulipua kwa mabomu shamba la rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe la kufugia ng’ombe na lenye kiwanda cha maziwa.

Watu hao wanakabiliwa na kula njama za kufanya hujuma, kutakatisha fedha kwa ajili ya kufanyia ugaidi na kuwa na silaha bila kibali.

Washitakiwa hao wanadaiwa kuwa wafuasi wa chama kimoja kidogo cha kisiasa, ambapo wawili miongoni mwao ni askari wa Jeshi la Ulinzi la Zimbabwe.

Inadaiwa kwamba kundi hilo lilikuwa limepanga kutumia mabomu ya petroli katika kushambulia shamba hilo la Mugabe lililo kaskazini mwa Harare, Ijumaa iliyopita.

Gazeti la serikali la Herald limesema watu hao walikamatwa na askari kanzu kabla ya kufanya shambulio hilo, lakini mwanasiasa wa upinzani, David Coltart, amesema hizo ni njama za siku zote za chama tawala nchini humo kupambana na wapinzani.

CHANZO: EYEWITNESS NEWS      ===>bit.ly/1TllZO7

Leave A Reply