Wanne mbaroni kwa kuhusika na kifo cha Mawazo

MAWAZO NEW

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Geita, Alphonce Mawazo enzi za uhai wake.

Jeshi la Polisi mkoani Geita linawashikilia watu wanne wanaodaiwa kuhusika na kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani humo, Alphonce Mawazo.

Kifo cha marehemu Mawazo kimetokea jana Jumamosi Novemba 14 majira ya saa sita mchana baada ya kuvamiwa na kundi la watu na kuanza kumshambulia kwa silaha za jadi.

Mawazo na lema_thumb[2]

Alphonce Mawazo akiwa na Godbless Lema.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema chanzo cha tukio hilo ni kwamba kulikuwa na mkutano wa ndani ya Chadema uliofanyika ukumbi wa Ludete B uliokuwa unahusu mambo yao ya uchaguzi na walipokuwa wanaendelea na kikao chao kuna mtu ambaye anadaiwa ni mfuasi wa Chadema alikuja na na kumnong’oneza marehemu Mawazo na baada ya hapo wajumbe walipata mshutuko na kutoka nje na wakakutana na kundi la watu na mtafaruku ulianzia hapo.

Ameongeza kuwa tatizo hilo kutokea kunahusishwa pia na itikadi za kisiasa lakini bado Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wake.

Hata hivyo Kamanda Mponjoli amesema hali ni nzuri maeneo ya Katoro hasa Kata ya Ludete ambapo uchaguzi wa diwani umefanyika leo.


Loading...

Toa comment