The House of Favourite Newspapers

WANNE WAUAWA KITONGOJI CHA MATHARE KENYA

0

Takriban watu wanne wamethibitishwa kuuawa wakati wa mashambulizi kwenye mtaa wa Mathare mjini Nairobi nchini Kenya

Wakazi wa mtaa huo wa mabanda wanadai kuwa makundi yaliyokuwa yamejihami kwa mapanga na silaha zingine yalivamia mtaa huo na kuwaua watu hao ambapo pia waliharibu mali.

Polisi wanasema kuwa wanachunguza chanzo cha mauaji hayo.

Wakazi wanasema waliamka kwa mshangao asubuhi walipoona miili ya watu wanne iliyokuwa na majeraha

 Mahakama yasikiliza kesi inayopinga uchaguzi wa Uhuru Kenyatta

 

Kuuawa kwa watu hao kumesababisha ghasia kusambaa hadi mitaa iliyo karibu huku polisi wakikabiliana na wale waliokuwa wakilalamikia mauaji hayo.

Kamanda wa polisi mjini Nairobi Japheth Koome alithibitisha mauaji hayo na kusema kuwa uchunguzi unafanywa, lakini akatupilia mbali madai kuwa yamesababishwa na ghasia za kikabila kufuatia hali ya kisiasa iliyopo sasa.

Mauaji hayo yanatokea siku moja baada ya watu wengine watano kuuawa wakati wa kumkaribisha kinara wa upinzani ambaye alikuwa ziarani Ulaya na Marekani.

Polisi wanasema kuwa waliouawa walikuwa ni wezi waliopigwa na raia wenye hasira kali.

Leave A Reply