The House of Favourite Newspapers

Wanyama Apewa Mtaa Dar, Ashuhudia FC Kauzu Ya Chifu Wa Masela Ikiteketea

0
Victor Wanyama (kushoto) akijadiliana jambo na meya wa Ubungo, Boniface Jacob

KIUNGO wa  Tottenham, Mkenya, Victor wa Nyama, amepewa heshima na serikali ya Wilaya Ubungo kwa kwa kuipa moja ya barabara za Ubungo jina la nyota huyo ambaye alikuwa mgeni wa heshima kwenye mchezo wa Ndondo Cup 2017 kati ya FC Kauzu dhidi ya Faru Jeuri.

Kiungo huyo wa Kimataifa wa Kenya alipata fursa ya kwenda kuizindua barabara hiyo ambayo kwa ipo kwenye matengenezo ikifanyiwa ukarabati ili kuwa katika kiwango kizuri ukilinganisha na sasa.

Madee akifutilia mchezo kati Faru Jeuri na FC Kauzu ukiendelea

Mara baada ya kukabidhiwa na uongozi wa wilaya hiyo nchini ya meya wa manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob, Wanyama alisema kuwa amefurahi kuona watu nje ya nchi yake wanamtambua na kumheshimu.

Kwa upande wa katika mchezo aliokaribishwa kama mgeni wa heshima, timu ya Faru Jeuri ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya FC Kauzu lilifungwa na Tumba Swedi kwenye dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza ambapo mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Kinesi, Dar.

Wanyama akiingia kukagua timu kabla ya mechi kuanza
Wanyama akiwa na kikosi cha timu ya Faru Jeuri
Wanyama akiwa na waamuzi wa mchezo
Wanyama akiwa na kikosi cha FC Kauzu

Wanyama akipokea cheti mara baada ya kuzindua mtaa wenyewe jina lake kutoka kwa viongozi wa Serikali ya Manispaa ya Ubungo

(Picha Musa Mateja na Ibrahim Mussa)

Leave A Reply