The House of Favourite Newspapers

Wanyama: Samatta Atafika Mbali

0
Straika Mtanzania, Mbwana Samatta atajituma zaidi katika timu yake ya KRC Genk ya Ubeligiji.

KIUNGO wa Tottenham Hotspur, Victor Wanyama amesema iwapo straika Mtanzania, Mbwana Samatta atajituma zaidi katika timu yake ya KRC Genk ya Ubeligiji, basi atafika mbali kisoka. Wanyama raia wa Kenya, yupo nchini kwa mapumziko akisubiri msimu ujao wa Ligi Kuu England ambao utaanza Agosti, mwaka huu.

Akizungumza kupitia kituo kimoja cha redio jijini Dar es Salaam, Wanyama alisema Samatta amefanya vizuri msimu uliopita na iwapo atajituma zaidi msimu ujao, kuna uwezekano wa kupata timu nyingine kubwa popote duniani.

Wanyama raia wa Kenya.

“Samatta amefanya vizuri sana msimu huu na akijitahidi kucheza vizuri zaidi msimu ujao atakuwa bora zaidi na ataweza kucheza timu yoyote kubwa duniani. “Kuhusu suala la

yeye kupata nafasi Genk amefungua njia kwa wachezaji wengine wa Tanzania kuweza kujituma ili kupata nafasi ya kutoka nje ya nchi ikiwezekana nje ya Afrika,” alisema Wanyama. Msimu uliopita, Samatta aliiwezesha Genk kufika robo fainali ya Europa League kabla ya kutolewa na Celta Vigo baada ya kufungwa mabao 4-3. Kwanza ilifungwa 3-2 halafu ikatoka sare ya bao 1-1.

STORI: KHADIJA MNGWAI | CHAMPIONI JUMAMOSI

Leave A Reply