Wanyarwanda Waunga Mkono Mabadiliko ya Katiba

rwanda (5)Rais wa Rwanda, Paul Kagame.

Wanyarwanda wameunga mkono kwa wingi marekebisho ya katiba ambayo yatamruhusu Rais Paul Kagame kuendelea kuongoza, matokeo ya awali ya kura ya maoni ya mabadiliko ya katiba iliyopigwa jana nchini humo yanaonesha hivyo.

rwanda (1)Raia akipiga kura.

Kwa mujibu wa taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Rwanda inasema, asilimia 98 ya wapiga kura wameunga mkono marekebisho hayo ya katiba ambayo yatamruhusu Rais Paul Kagame kuwania kwa muhula mwingine mwaka 2017, baada yake kumaliza muhula wa pili.

rwanda (2)Wanyarwanda walivyopiga kura ya mabadiliko ya katiba jana.

Tume hiyo imesema wilaya 21 kati ya wilaya 30 zimechapisha matokeo yake kufikia sasa. Matokeo kamili yatatolewa baadaye leo Jumamosi.


Loading...

Toa comment