WAOGOPE WANAWAKE WA AINA HII !

KATIKA kuangalia tabia za wanawake, ni vyema ukawa chonjo kwani ukiingia chaka wanaweza kuyafanya maisha yako ya uhusiano kuwa balaa. Labda saa hizi uko katika uhusiano wa muda mrefu na mpenzi wako au sasa hizi uko mbioni unatafuta, kuwa macho na aina hii ya wanawake ambao wanaweza kukuharibia au kukuletea shida katika uhusiano wako nao mbeleni;

1: MTUMIAJI

Kuna aina ya wanawake ambao wanakuona wewe kama mwanaume mzuri ili wakutumie kama chambo. Unaweza kuwa mwanamume ambaye unauunganishi na watu wengi. Mwanamke wa aina hii ataona kuwa akiwa karibu na wewe itakuwa rahisi kwake kupata “connection” na marafiki zako.

Hii ina maana kuwa pindi mwanamke wa aina hii akifanikiwa kupata anachokitafuta, bila kupoteza wakati atakutema.

2: ASIYEOMBA MSAMAHA

Huyu ni aina ya wanawake ambao hawawezi kuomba msamaha kwa jambo lolote ambalo wamefanya hata kama ni la makosa kiasi gani. Mwanamke wa aina hii anaweza kuomba msahamaha kwa shingo upande au aamue kunyamaza kwa jambo alilofanya la kukwaza. Aina hii ya wanawake haifai kwani mtu ambaye hakubali makosa yake si mtu mzuri wa kuishi naye.

3: MLALAMISHI

Huyu ni aina ya mwanamke ambaye nyakati zote yeye hulalamikia kuhusu hili na lile. Yaani kwake hakuna jambo zuri. Atakuwa akilalamika kuhusu marafiki zake, maisha yake ya kila siku nk. Yaani yeye siku zote hana amani. Aina hii ya mwanamke haifai kabisa kwani ulalamishi wake wa kila siku utakuchosha kwa haraka. Lakini pia lawama hazitaishia, atakulalamikia hata kama wewe utamfanyia jambo zuri kiasi gani.

4: ASIYEJIELEWA

Huyu ni mwanamke ambaye haelewi anachotaka maishani (mtaka yote). Wakati wote yeye atakuwa anahangaika na uchaguzi wake na hajiamini. Aina hii ya mwanamke achana nayo kwa sababu wewe pia inamaanisha hayuko asilimia mia moja kama aendelee kuwa nawe au la.

Mara nyingi mwanamke wa aina hii huwa na wanaume wengi na ni rahisi kwake kukuendea kinyume kimapenzi.

5: ASIYETOSHEKA

Hii ni aina ya mwanamke ambaye anatarajia makuu kila wakati na hatosheki. Anapenda kutawala na kila kitu anataka kifanywe vile ambavyo anataka. Najua wanawake wanapenda wanaume ambao ni gentlement, lakini baada ya muda mfupi utakuja kugundua kwamba aina hii ya mwanamke watakufanya bwege muda unaposongea, yaani watakukalia kichwani.

6: MWENYE KUKASHFU

Kuwa na maoni na kukashfu si jambo baya kwani kukosoa mambo katika uhusiano ni jambo zuri. Lakini usizidishe. Aina hii ya wanawake wanaokashfu kupitia kiasi ni wale ambao wakisema jambo fulani, basi litabakia hilohilo na hata ufanyeje hawawezi kugeuza.

7: NUSANUSA

Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye haipiti siku bila kukuchunguza. Kila wakati anapopata mwanya anajaribu kukuchunguza miondoko yako. Unaweza kuwa mwaminifu kwake, lakini yeye bila kutosheka lazima akuchunguzechunguze, mara aangalie simu yako, atake kujua umetoka wapi, umeenda wapi, jana ulivaa nguo gani, anawauliza maswali marafiki zako kukuhusu nk. Aina hii ya mwanamke muogope sana kwani pia yeye haaminiki. Hivyo mara nyingi ukiona mwanamke anashindwa kukuamini kwenye uhusiano, inamaanisha kuwa pia yeye ana hilo tatizo.

8: ASIYE NA MAONO

Aina hii ya mwanamke inafanana karibu na ile ya asiyejielewa, lakini hii ni kuwa hana maoni kujihusu yeye mwenyewe. Ukimuuliza chochote anakwambia kuwa hajui au hana mtazamo wowote. Mwanamke huyu anaweza kuonekana mwanamke mzuri mara ya kwanza kwa sababu hawezi kukupinga kwa unachosema, lakini pindi muda unaposogea utaona kuwa ataanza kuwa mzigo.

9: MCHEZA NDONDI

Hii ni aina ya mwanamke ambaye anakasirika kwa haraka na akichukizwa, chochote kinachokuja akilini mwake ni vita.

10: MTOTO WA MAMA

Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye hatafanya chochote bila kuingiza wazazi wake katika maongezi yake. Aina hii ya mwanamke ni mbaya kwa sababu mwanamke hata ufanye nini, lazima aingize wazazi wake. Hii inamaanisha kuwa hawezi kudhamini maoni yako kab


Loading...

Toa comment