The House of Favourite Newspapers

Waoo…! Kama Jana Vile!-17

0

ILIPOISHIA RISASI JUMAMOSI:

“Ni sawa ndiyo, wala hakuna shida. Mi nisichotaka ni kuongozana tu,” alisema Magembe.

“Basi anza kutoka wewe,” Magembe alimtaka mama Monica atangulie huku akimkatia kitita cha shilingi laki moja mwanamke huyo.

Mlio wa mlango, uliwashtua wale wanaume kwenye vyumba vingine, wakatoka haraka sana…

JIACHIE MWENYEWE SASA…

Kila mmoja alitaka kumwona mwanamke aliyekuwa akiwasisimua kimahaba kwa maneno matamu kutokea chumbani.

Mama Monica alipotoka tu, akashtuka sana kukutana  uso kwa uso na kaka yake mkubwa kuzaliwa kwao. Ni miongoni mwa hao wanaume wawili waliohamasishwa na sauti za mahaba za kwake…

“Ha! Kaka…” alihamaki mama Monica huku miguu ikiwa imeganda kama mtu aliyenaswa na umeme.

“Wewe umefuata nini huku gesti?” aliuliza kaka mtu huyo kwa sauti iliyoishiwa nguvu. Moyoni aliwaza…

“Inamaana kwamba, saa zile nilikuwa nahamasishwa na dada yangu mwenyewe?” alijiuliza kaka wa mama Monica huku uso wake ukiwa umebadilika rangi kwa kuchukia pia kwa aibu. Mtu na dada yake kukutana gesti ni tukio la ajabu sana.

“Kuna…kuna…mkaka nilikuja ku…kumwona,” mama Monica alijitetea huku akitetemeka sauti…

“Unajua unanidanganya mtu mzima na akili zangu?”

Mama Monica alinyamaza. Alibaki akimwangalia kaka yake.

Moyoni alijuta mara ya pili kuhusu shateni. Awali alimkubalia mwanaume huyo akiwa hajui lolote lakini sasa kama hatari inamwelemea.

***

Kule chumbani, Magembe alishasikia kila kitu kilichotokea nje. Kwa hiyo akasita kutoka…

“Mh! Lakini na wao bwana wamezidi. Kaka moto chini, dada moto bati…sasa nani mwenye nafuu kati yao?” alijiuliza Magembe.

Nje, mjadala kati na mama Monica na kaka yake uliendelea kwa kasi. Yule mwanaume mwingine aliyetoka sambamba na kaka yake mama Monica yeye alishajifungia ndani baada ya kubaini kuwa, mtu na kaka yake wamefumaniana.

“Ina maana mumeo anajua uko hapa?” kaka wa mama Monica alimuuliza mdogo wake huyo.

“Hapana kaka.”

“Sasa unadhani akikuona nini kitatokea?”

Mama Monica alibaki ameinamisha kichwa huku akipepesa macho chini.

Kwa hasira,  kaka huyo alirudi chumbani huku akitingisha kichwa kulia na kushoto…

“Baby kwani kuna nini? Maana nimekuona umetoka haraka na ghafla nasikia mzozo,” alisema Maria, mmoja wa mademu walioitwa kutokana na uhamasishaji wa mama Monica…

“Ah! Kuna wakati nilisikia sauti kama ya mdogo wangu, nikawa nafuatilia. Sasa nimetoka nakuta ni kweli yeye,” alisema kaka mtu.

“He! Sasa? Kwani si msela tu…au ana mume?”

“Siyo mume tu, tena wa ndoa. Wana mtoto anaitwa Monica. Yaani namwonna dada yangu akiipoteza ndoa yake hivihivi.”

“Kwani yeye anajiteteaje?” aliuliza Maria.

“Unadhani atajiteteaje? Anasema kuna mtu alikuja kumwona. Hivi Maria, kwani siku hizi kuna watu  bado wanaonania gesti? Si afadhali ingekuwa baa.”

***

Mama Monica akiwa njiani anaelekea nyumbani kwake, miguu ilikuwa mizito. Kwanza alipotoka tu nje ya gesti hiyo alimtumia meseji Magembe…

“Usitoke nje, kuna soo. Nimekutana na kaka yangu. Nadhani atataka kukujua wewe ni nani!”

“Poa. Nimeshtukia ishu mbona, nipo ndani,” alisema Magembe akijikomelea zaidi na kitasa.

***

Akiwa nyumbani, mama Monica alikuwa akitatizwa na swali moja ambalo lilikosa majibu.

“Je, kaka anaweza kuja kumwambia baba Monica kwamba ameniona nikitoka gesti?

“Mh! Sidhani….yaani kaka yangu, tena wa tumbo moja  aje afanye ushabiki mpaka mimi niachike. Lakini kweli maneno mengine ya wahenga yana ukweli f’laini.”

***

Sasa ilikuwa zamu ya Magembe kutoka kwenye gesti hiyo kwani ukweli ni kwamba, ukimya ulipotawala sana  nje, Magembe akajua kumetulia. Alikuwa amevaa nguo zote hadi viatu. Akafungua mlango polepole na kuanza kwa kuchungulia nje kwanza.

Alipojiridhisha kwamba hakuna mpangaji aliyefungua mlango wa chumba chake, alianza kutoa  mguu mmoja baada ya mwingine kwenda nje.

***

Ilikuwa bahati mbaya sana kwani wakati Magembe anatoka kwa kujichungachunga, kaka wa mama Monica naye akawa anatoka sijui kwa ajili ya kwenda wapi!  Wakakutana macho…

“Ha! Magembe…”

“Ha! Daudi…”

 Je, nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Risasi, Jumatano ijayo.

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!

Leave A Reply