The House of Favourite Newspapers

Waoo…! Kama Jana Vile!-18

0

ILIPOISHIA RISASI JUMATANO:

Waliangaliana kwanza japokuwa kulikuwa na giza zito, mama Monica akacheka kidogo kwa sauti, Magembe akaachia tabasamu. Lakini mara mlango ukagongwa kwa ustaarabu sana…

“Ngo…ngo…ngo!”

Wawili hao walikuwa wamekumbatiana, lakini waliposikia mlango umegongwa wakaachana na kuanza kuogopa…

“Atakuwa nani?” aliuliza mama Monica…

“Eti nani?” aliuliza kwa sauti Magembe…

JIACHIE MWENYEWE…

“Mimi bro…”

“Wewe nani?”

“Naitwa Onesmo.”

“Onesmo! Onesmo gani na unataka nini? Mimi unanijua?”

“Sikujui bro ila nina shida na wewe…”

“Shida gani?”

“Ungetoka basi bro tuzungumze,” alisema huyo Onesmo…

“Baby, unajua huku ni uswahilini sana…sasa mtu usiyemjua anakuita halafu wewe unatoka, sidhani kama ni sawasawa,” alisema mama Monica.

“Si sawasawa lakini unadhani tutatokaje humu ndani? Maana kama yupo mlangoni na ana shida na mimi maana yake hatatoka,” alisema Magembe.

“Kwani yeye ana shida na wewe au ana shida na mtu mwingine yeyote aliye kwenye gesti hii?” mama Monica aliuliza swali la msingi sana…

“Eti…una shida na mimi au na mtu yeyote wa kwenye gesti hii?”

“Wewe broo…wewe si ndiyo umeingia humo ndani na demu muda si mrefu!”

“Huyu demu unamjua?”

“Simjui.”

“Khaa! Sasa wewe una shida gani kwani?”

“Bro ungetoka tuzungumze.”

“Je, akitoka huyu demu?” aliuliza Magembe na kusubiri jibu kwa hamu kubwa…

“Hapana, inatakiwa wewe.”

Magembe alipiga moyo konde, akavaa nguo na kutoka. Moyoni alisema liwalo na liwe…

“He! Baby unakwenda?” aliuliza mama Monica…

“Nakwenda, we subiri ndani.”

Alifungua mlango Magembe, akatoka huku akifunga mlango kwa nyuma. Mbele yake akakutana na vijana watatu ambao walimuonesha sura ya tabasamu…

“Bro samahani bwana, unajua wenzako tunaishi kwa kutegemea wanaume kama nyinyi,” alisema kijana mmoja aliyejitambulisha kuwa ndiye Onesmo…

“Kivipi?” alihoji Magembe huku uso wake ukiweka alama ya kujiuliza maswali kibao…

“Yaani sisi hatuna mademu wala nini! Sasa kwenye gesti hii akiingia mwanaume na demu wake huwa tunapiga chabo wakati wanacheza mechi mpaka na sisi tunajiridhisha. Sasa wewe ulipozima taa inakuwa ngumu sisi kuona, ndiyo maana tukakuita tuzungumze kwamba chondechonde usizime taa ili na sisi tuburudike kidogo.”

Magembe alihema kwa nguvu zake zote huku akiwatumbulia macho wale vijana kama anayejiuliza hivi wana akili kweli!

Aligeuza kurudi ndani bila kuwajibu lolote…

“Anasemaje?” mama Monica alimdaka na swali…

“Ah! Wapuuzi sana aisee…eti wanataka niwape hela, hawajala,” alisema Magembe…

“Kwani wako wangapi?”

“Watatu.”

“He! Asee, kweli huku ni uswahilini.”

Magembe alimsimamisha mama Monica, wakaendelea kudendeka huku wakigugumia. Lakini ghafla Magembe akaingiwa na wazo kwamba, mama Monica si mkewe, kwani akiwasha taa ili wale vijana nje waone kuna nini? Akawasha taa!

“He! Kwani wameondoka?” aliuliza mama Monica…

“Wameondoka muda uleule mbona.”

Basi, waliendelea kudendeka mpaka mama Monica akazidiwa nguvu akiwa amesimama, mwenyewe akatangulia kitandani na kupanda, akalala tayaritayari…

“Njoo baby bwana,” alisema mama Monica.

Kule nje, wale vijana hawakuondoka. Walipoona taa imewashwa, wote wakasogea mlangoni na kuanza kuchungulia kwa uangalifu mkuu ili wasijulikane. Waliamini Magembe aliwasha taa kwa makusudi ili wao wafaidi…

“Jamani hakuna kuliza kandambili chini, sawa?” alisema Onesmo.

Walikaza macho ndani.”

Mama Monica na Magembe walizama kwenye mechi, mama Monica kama kawaida yake alianza mbwembwe za mahaba kiasi cha kelele zake kufika nje kwa wale vijana hali iliyowalazimu waanze kuweweseka.

Magembe alikuwa anaongeza spidi na kupunguza, anaongeza na kupunguza. Wale vijana nao wakawa wanakwenda naye sambamba lakini walitaka sana Magembe akaze mwendo ili wao wamalize…

“Bro si uongeze spidi moja kwa  moja tu ijulikane moja.”

Je, nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Risasi, Jumatano ijayo.

Leave A Reply