Waoo…! Kama Jana Vile!-9

ILIPOISHIA RISASI JUMATANO:

Dakika moja baada ya wale wamachinga kuondoka, mama Monica akamuegemea begani Magembe na kumwambia…

SHUKA NAYO MWENYEWE…

“Uko bize sana?”

“Wala, vipi kwani?”

“Tutafute gesti tukalale mpaka kigiza cha saa mbili ndiyo tutoke,” alisema mama Monica huku akilegeza macho.

Kifupi mama Monica alishakwisha katika kila idara. Mambo makuu aliyokuwa akifanyiwa na Magembe yalimbadilisha akili kiasi kwamba, hakuweza kuweka shingo ngumu tena…

“Nikwambie kitu mama Monica…”

“Niambie mpenzi wangu.”

“Uliposema wewe ni mke wa mtu na hujawahi kusaliti na mimi nikaamua kukubaliana na wewe. Niliuondoa moyo wa kukupenda nikauweka wa kukuheshimu kama mwanamke mwenye maadili na kujitambua. Baadhi ya wanawake hawajitambui hata kidogo. wamekuwa wakiamini wao wanaweza kutumikia mabwana wawili wakati siyo,” alisema kwa hisia Magembe.

“Kwa hiyo umeamua mwenyewe tuwe ndugu?”

“Nimeamua hivyo kutoka moyoni…”

“Pafyumu…anti pafyumu,” machinga mwingine alipita na kunadi biashara yake mbele ya wawili hao…

“Hebu pafyumu wewe,” alisema Megembe.

Chinga akazitoa na zilizomo ndani ya mfuko mkubwa, akamwonesha Magembe kwa kumpulizia moja baada ya nyingine…

“Psiii…psiii,” alijipulizia naye Magembe kisha akampa mama Monica pafyumu mbili za aina moja…

“Hebu nusa hizo…nahisi harufu yake ni nzuri sana,” alisema. Mama Monica alipuliza kidogo kwenye kiganja, akatingisha kichwa kukubali kwamba kweli zina harufu nzuri…

“Hizi zote bei gani?” aliuliza Magembe…

“Elfu arobaini.”

Magembe alilala ubavu, akatoa waleti, akachomoa wekundu wanne na kumpa muuzaji. Mama Monica akabaki ameduwaa nazo…

“Sasa utaziweka wapi? Au nikuwekee kwenye mkoba wangu mpaka wakati unaondoka?” aliuliza mama Monica…

“Hapana, ni zako hizo nimekununulia wewe,” alisema Magembe.

Mama Monica aliishiwa nguvu kabisa…

“Waoo, jamani. Halafu nilikuwa sina pafyumu kabisa tangu mwezi uliopita,” alisema mama Monica huku akimwegemea tena mwanaume huyo…

“Mpenzi,” aliita mama Monica.

“Niambie mama Monica…”

“Twende gesti bwana. Basi mara moja tu leo, halafu basi. Yaani kwa upande wangu hiyo ndiyo zawadi pekee ya kukupa.”

Moyoni Magembe alifurahia sana na kusema…

“Sasa we unadhani kukumwagia mazawadi yote haya mwisho wake ni nini? Una kichaa nini?”

Lakini kwa sauti akasema…

“Tukubaliane kitu kimoja, leo tu. Lakini baada ya hapo kila mtu na hamsini zake!”

“Sawa, nakubali,” alisema mama Monica.

“Basi ngoja nitoke nikatafute chumba halafu nitakushtua, sawa?” alisema Magembe akiwa anasimama huku akitupa mezani shilingi elfu kumi na tano kwa ajili ya kulipia vinywaji wakati bili yenyewe ilikuwa haizidi hata elfu nane.

Magembe alitoka nje, akaulizia kwa madereva wa bodaboda kama pana gesti jirani, akaoneshwa. Akaenda, akachukua chumba, akampigia simu mama Monica na kumpa maelekezo.

Mama Monica kwa vile alishakunywa bia mbili, alichangamka kwa mbali, akasimama huku moyoni akisema…

“Hivi kweli leo mimi mama Monica nakwenda kusaliti? Mume wanghu hatajua kweli? Yaani nakwenda kuchinjwa kirahisirahisi hivihivi? Ama kweli Megembe kaniloga.”

Mama Monica alikuwa hajazoea kuingia gesti. Akazama ndani akihisi mwili kumsisimka. Akaingia mpaka kwenye chumba alichoelekezwa, alimkuta Magembe ameshavua nguo zote na amevaa taulo la gesti huku maiki ikiwa ina umeme tayari.

Ilibidi mama Monica avumilie ili aweze kumridhisha mwanaume huyo ambaye kwake mpaka muda huo aliona amemtendea mambo makubwa kiasi kwamba, hata haamini kama kulala naye kulikuwa ni zawadi kubwa.

“Yaani umevua kabisa?” aliuliza mama Monica huku macho yake yakikaza chini kwa aibu…

“Kwani humu ndani kuna ishu nyingine zaidi ya kilichotuleta mama Monica?”

“Na kweli hakuna…teh! Teh! Teh!” Alisema akicheka mama Monica na yeye akaanza kuchojoa moja baada ya nyingine huku aibuaibu ya mbali ikitawala sura yake nzuri…

“Lakini wewe Magembe bwana, yaani umetumia njia ya ujanja sana kuninasa.”

“Hamna, si nimekwambia nilishasalimu amri we mwenyewe ndiyo umeng’ang’ania, sasa mimi  nifanyeje mama Monica. Au tuache?” aliuliza Magembe…

“Noo noo! Mi nimeshachaji tayari jamani, nipe haki yangu ijulikane moja,” mama Monica alisema kwa kulalamika.

Je, nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Risasi, Jumatano ijayo.


Loading...

Toa comment