The House of Favourite Newspapers

ads

Wapalestina Tisa Wauawa katika Uvamizi wa Israel huko Jenin

0

Wapalestina tisa, akiwemo mwanamke mzee, wameuawa katika uvamizi wa kijeshi wa Israel katika ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, maafisa wa Palestina wanasema.

Waziri wa afya wa Palestina alionya kwamba hali ni “mbaya” huko Jenin, huku watu wengine wengi wakijeruhiwa na gari la wagonjwa kushindwa kuwafikia.

Wodi ya watoto ya hospitali ya eneo hilo ilipigwa na mabomu ya machozi ya Israeli, alisema.

Jeshi la Israel lilitoa maelezo machache, lakini vyombo vya habari vya Israel vilisema kuwa lilichukua hatua ya kuzuia “shambulio kubwa” la wanamgambo.

Kundi la wanamgambo wa Palestina Hamas na Islamic Jihad walisema walikuwa wakipambana na wanajeshi wa Israel katika mji huo, ambapo kumekuwa na uvamizi wa mara kwa mara wa Israel.

Mvutano umeongezeka hivi karibuni katika Ukingo wa Magharibi huku jeshi la Israel likiendelea na kile inachoeleza kuwa ni mashambulizi dhidi ya ugaidi.

Takriban Wapalestina 28 wameuawa na wanajeshi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi hadi sasa mwaka huu, wakiwemo wanamgambo na raia.

Mwaka jana, zaidi ya Wapalestina 150 waliuawa, karibu wote na wanajeshi wa Israel, huku msururu wa mashambulizi ya Wapalestina yakiwalenga Waisraeli, pamoja na kuwafyatulia risasi wanajeshi wakati wa mashambulizi ya kuwakamata, yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 30, wakiwemo raia, polisi na wanajeshi.

NANI ni NANI MKEKA MPYA wa MA-DC wa RAIS SAMIA, WENGINE WAHAMISHWA WILAYA…

Leave A Reply