The House of Favourite Newspapers

Wapelelezi wapewa mbinu mpya kukabiliana na uhalifu mtandaoni

0

 

Wapelelezi wa Jeshi la Polisi hapa Nchini wapewa mbinu ya namna ya kukabiliana na uhalifu mtaandaoni.

Mafunzo hayo yamefunguliwa leo march 06 2023 na kamishina wa Polisi CP RAMADHAN KINGAI ambaye pia ni Mkurungezi wa makosa ya jinai nchini, katika shule ya Polisi Tanzania Moshi Mkoani kilimanjaro ambapo amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo mkubwa wapelelezi kukabiliana na makosa ya kifedha.

Kingai amesema bainisha kuwa makosa mengi kwa sasa yanatendeka kwa teknolojia ya hali ya juu na kuwaomba washiriki kuyapokea mamfunzo hayo na kujikita Zaidi kujifunza nakupata mbinu mpya katika kukabiliana na matukio ya yanayofanywa kwa sayansi na teknolojia hapa Nchini ambapo amesema kukua kwa sayansi na teknolojia kumepelekea watu wasio waadilifu kufanya uhalifu nakubainisha kuwa Jeshi hilo halite wafumbia mcho wahalifu hao.

 

 

Sambamba na hilo amebainisha kuwa washiriki watajifunza kuhusu taratibu za Ukusanyaji wa ushahidi, mpango wa upelelezi na dhana nzima ya utaifishaji na urejeshaji wa mali zinazotokana na uhalifu. Upelelezi sambamba wa kifedha (Parallel Financial Investigation) na ufuatiliaji wa mapema wa mali zinazotokana na Uhalifu.

Kwa upande wake Mkuu kitengo cha upelelezi wa makosa ya kifedha kutoka kutoka makao makuu ya Jeshi hilo Kamishina msaidizi wa mwandamizi wa Polisi SACP CHARLES ULAYA amesema lengo la mafunzo hayo ni kujifunza namna ya kupambana nauhalifu na wahallifu hao na kuongeza uwezo wa upelelezi na kubadilishana Uzoefu na mahusiano wa tasisi mbali mbali Pamoja na wadau katika kufanikisha mapambano ya uhalifu huo wa kimtandao.

 

Amebainisha kuwa wahalifu siku zote wamekuwa wakipanga mbinu mpya amesema Jeshi hilo nalo liko msatari wa mbele kukabiliana na wahalifu hao ambao wanarudisha nyuma maendeleo ya Nchi.

Pia amelishukuru shirika lisilo la kiserikali la PAMS Foundation kwa kuona umuhimu wa kufadhili mafunzo hayo kwa wa wapelelezi nchini. PAMS Foundation ambayo imekuwa na mchango mkubwa wa kutoa mchango mkubwa katika maswala ya ulinzi.

Leave A Reply