Wapinzani Wa Yanga Waiba Mbinu Wafichua Watakavyowabana
WAPINZANI wa Yanga ndani ya Ligi Kuu Bara kuelekea kwenye mchezo wao unaotarajiwa kuchezwa Aprili 21 2025 Uwanja wa Tanzanite, Kwaraa Fountain Gate wamebainisha kuwa wamepata mbinu za wapinzani wao hivyo wanajua namna watakavyofanya kazi kuwadhibiti.
Yanga ni vinara ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya mechi 25 ni pointi 67 wamekusanya kibindoni na safu ya ushambuliaji imetupia jumla ya mabao 64 ikiwa ni safu kali kwenye kumalizia nafasi ambazo zinatengenezwa ndani ya uwanja kwenye ligi.
Inakutana na Fountain Gate ambayo namba mbili kwa timu ambazo zimeruhusu mabao mengi ndani ya ligi ambayo ni 47 baada yakucheza mechi 26 ikiwa nafasi ya 9 na pointi zake kibindoni ni 29.
Issa Mbuzi amesema kuwa wanatambua ubora wa Yanga ulipo na udhaifu kwa kuwa waliwatazama kwa ukaribu
kwenye mchezo dhidi ya Stand United uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex, Aprili 15 2025 na ubao ukasoma Yanga 8-1 Stand United.
“Tunawatambua vizuri hawa Yanga na kwenye mchezo wao dhidi ya Stand tulikuwa na wataalamu wakusoma mbinu zaidi ya wanne, wameniambia wameona namna itakayotupa matokeo kwenye mchezo wetu Aprili 21 tukiwa nyumbani.
“Eneo la kiungo kuna matatizo pale na wanaye Aziz Ki ambaye huyu tutampa mtu wakutembea naye hatua kwa hatua ndani ya uwanja, utakuwa mchezo mgumu lakini tunahitaji pointi tatu zao ili tujihakikishie nafasi ya sita kwenye msimamo.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.