Warda aanika vigezo vya mumewe
Na Dustanshekidele, Moro
KAZI ni kwako! Mtangazaji ‘the big name’ mjini hapa anayekimbiza na kipindi chake cha Mcharuko wa Pwani kwenye Radio Planet FM, Warda Makongwa ameanika vigezo vya mumewe mtarajiwa.
Wakati wa bethidei yake wiki iliyopita, Warda aliliambia Ijumaa Wikienda anataka mume ambaye ni mcha Mungu, mchapakazi,anayetekeleza vyema majukumu yake kwa mke na asiwe mlevi.