The House of Favourite Newspapers

Video: Warda Afichua Siri Ya Kutoroka – Azungumza Kila Kitu Amwaga Machozi

Mtoto Warda Mohamed (15), mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Nyumbu iliyopo Kibaha mkoani Pwani, ambaye alipotea tangu Aprili 19, 2023, amepatikana ambapo leo amekutanishwa na mama yake mzazi na kueleza sababu iliyomfanya atoroke kwa mlezi wake.

Tukio la kukutanishwa kwa Warda na mama yake, limefanyika katika ofisi za Global TV, Sinza Mori jijini Dar es Salaam.

Kampeni ya kumtafuta Warda, ilikuwa ikiongozwa na mtangazaji @zali_mapito na timu nzima ya Kipindi cha #Mapito kinachorushwa kupitia @255globalradio na @globaltvonline.