Warda Aomba Kurudi Shule – ”Nisameheni, Mumepata Tabu Kunitafuta”…
Mtoto Warda Mohamed (15), mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Nyumbu iliyopo Kibaha mkoani Pwani, ambaye alipotea tangu April 19, 2023 na kupatikana Oktoba 28, 2023 amesema anataka kurudi shule na kuendelea na masomo.
Hata hivyo, Warda amesema anataka apelekwe kwenye shule nyingine tofauti na aliyokuwa akisoma awali, na ikiwezekana iwe shule ya bweni ambapo atasoma kwa bidii.
Warda ameyasema hayo kupitia kipindi cha #Mapito ambacho ndicho kilichoongoza kampeni ya kumtafuta, chini ya mtangazaji wake, @zali_mapito na timu nzima ya @255globalradio na @globaltvonline.