Warembo Wajiachia Red Carpet Miss Kinondi – Pichaz + Video

 

USIKU wa kuamkia leo palikuwa hapatoshi pale katika Ukumbi wa The Life, Mwenge jijini Dar es Salaam ambapo kulikuwa na hafla ya mchuano mkali wa warembo waliokuwa wakiwania kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kutwaa taji la Miss Kinondoni.

 

 

Katika tamasha hilo, lengo kubwa lilikuwa ni kupata warembo watano ambao watachuana kwenye fainali ya kuwania taji la Miss Kinondoni ambayo itafanyika Jumamosi ijayo, Julai 13, 2019.

 

 

Tamasha lilinogeshwa na msanii wa ‘machejo’ ya singeli nchini maarufu kama Dulla Makabila na wasanii wengine huku mdhamini wa shindano hilo akiwa ni kituo cha Redio namba moja ya mtandaoni Tanzania kwa sasa, +255 Global Radio.

 

 

Warembo hao walipata fursa ya kuonyesha vipaji vyao ikiwa ni pamoja na kucheza, kuimba, kuchora, kuigiza, mitindo. mashairi na vipaji vingine kibao.

 

 

Walioshinda na kuingia katika hatua ya tano bora ni:  Conhellen Simba, Christina Andrew, Winnie Mbise , Leah Josephat na Juliana Joseph.

 

TAZAMA TUKIO ZIMA

Loading...

Toa comment