The House of Favourite Newspapers

WAREMBO WATAKAOTIKISA MISS TANZANIA 2018 NI SHIDA

Warembo hao wakiwasili kwenye Ofisi za Global Group, Sinza Mori jijini Dar es Salaam.
WAREMBO ambao wanashiriki katika Shindano la Miss Tanzania 2018, leo Alhamisi, Agosti 30, wametembelea makao makuu ya ofisi za Makampuni ya Global Group na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na makampuni hayo ikiwemo uzalishaji wa magazeti.
Wakisani katika kitabu cha wageni kwenye chumba cha mapokezi.
Walimbwende hao walifika katika Ofisi za Global Group ambazo ndani yake kuna Kampuni ya Global Publishers, wachapishaji wa magazeti ya Kiswahili yanayoongoza kwa habari za michezo nchini ya Championi na Spoti Xtra.
Wakiwa katika picha ya pamoja.
Mbali na kujionea uzalishaji wa magazeti pendwa ya Ijumaa, Risasi, Uwazi, Amani na Ijumaa Wikienda, pia walipata nafasi ya kutembelea studio za Global TV Online na kufanya mahojiano ambayo baadaye utayatazama kupitia YouTube channel ya Global TV.

Wakizungumza na Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho ofisini kwake.


 

Wakitazama kurasa nzuri za Gazeti Bora la Burudani na stori za mastaa, Gazeti la Ijumaa.

 

Mhariri wa Gazeti la Championi, Philip Nkini akiwatambulisha warembo hao kwa wahariri na waandishi.

 

Comments are closed.