The House of Favourite Newspapers

Wasafi.com ni Mtego kwa Mastaa Bongo

MAKALA: BONIPHACE NGUMIJE | UWAZI |SHOW BIZ

 AGOSTI 2, 2016 staa mwenye jina kubwa ulimwenguni Shawn Carter ‘Jay Z’ alitimiza malengo yake ya muda mrefu kwa kuwa msanii wa kwanza duniani kumiliki mtandao ambao umewawezesha waandishi wa muziki na wanamuziki mastaa wakubwa duniani kufaidika na jasho lao kwa kuuza kazi zao za audio na video kwa mashabiki wao duniani kote.

 

Jay Z

Mtandao huo unaitwa Tidal ambao ulianzishwa mwaka 2014 na Kampuni ya Kiswedishi iitwayo Aspiro, baadaye ukamilikiwa na Project Panther Bidco L.T.D kabla ya Jay Z kuununua mtandao huo ambao mpaka sasa una zaidi ya nyimbo milioni ishirini na tano (25) za audio na zaidi ya video elfu themanini na tano (85) huku mastaa wakiwemo Drake, DJ Khaled, Fat Joe, Nick Minaj na wengine wengi wakiweka kazi zao na kukunja mkwanja wa maana.

 

Diamond Platinumz

Huyo ndiye Jay Z, aliyemhamasisha mwanamuziki mwenye mafanikio makubwa Bongo, Diamond Platnumz kuwa msanii wa kwanza Tanzania kumiliki mtandao wake unaoitwa www. wasafi. com ambao unawawezesha wanamuziki kuweka kazi zao za audio na video huku wakiziuza kwa shilingi 300, ambapo mpaka sasa baadhi ya mastaa waliojitokeza na kuweka kazi zao ni pamoja na Profesa J, Navy Kenzo, Bill Nas, Ray C, Barnaba, Belle 9, Chegge na Temba.

Harmonize

Tofauti ya Jay Z na Diamond ni kwamba, Mmarekani huyo alipoununua Mtandao wa Tidal, malengo yake makubwa ni kuuza muziki na kuwasapoti wasanii wenzake kisha kila mmoja kupiga mkwanja, kwa wanaokumbuka hata kauli mbiu ya kuutangaza mtandao huo ilikuwa ni Tidal For All kwa tafsiri isiyo rasmi ni kwamba Tidal ni kwa ajili ya watu wote. Ukirudi kwa Diamond kinachoonekana nyuma ya mtandao wake wa www. wasafi.com ni mtego kwa mastaa Bongo, yaani anawasaidia kuuza kazi zao lakini wao wanatangaza lebo yake, wasanii wake na biashara zake zote zenye nembo ya wasafi.

Hili halionekani kwa Jay Z ambaye ana lebo yake ya Roc- A- Fella Records na Kampuni ya Roc Nation. Maana angeweza kuubadilisha Mtandao wa Tidal na kuita jina mojawapo la hayo ya kampuni zake kisha kujitangaza zaidi duniani kupitia wasanii ambao wameweka kazi zao kwenye mtandao huo.

Queen Darlin

Lakini kwa upande wa Diamond, mtego huo unaweza kuuona pale ambapo wasanii walioweka nyimbo zao kwenye mtandao huo wanapokuwa wanatangaza zinapatikana wapi! Lazima waseme katika Mtandao wa www.wasafi.com ambao unamilikiwa na Diamond Platnumz ambapo huko pia matangazo ya biashara zake ameweka.

 

Kwa hiyo kutokana na ukweli huu, baada ya miaka mitano mbele kama Diamond akifanikiwa kuutangaza mtandao huu vizuri na wasanii wengi kuweka nyimbo zao, asilimia 85 ya wanamuziki Bongo watakuwa wanamtangaza yeye, vijana wake na biashara zake. Ndiyo mahesabu ya kibiashara yanayoonekana katika mtandao wake.

Chege na Tema

Ni ukweli aweke kazi zake kwenye mtandao wake, inaweza kuwa ni kweli lakini katika sura nyingine, anatafuta urafiki wa kibiashara. Ili Kiba aingie mkenge na baadaye kuwa wakala wake wa kumtangaza, wasanii wake pamoja na biashara zake zingine kwa maana mashabiki wakimfuata Ali Kiba www. wasafi. com wanakuwa wamemfuata Diamond Platnumz. Unaweza kukumbuka pia Diamond alivyoua ushindani baina yake na Rich Mavoko pale tu alipomfanya kuwa msanii wake.

 

Hata hivyo, ninampongeza Diamond kwa maono yake, anaitendea haki ile kauli inayosema mwenye nacho ataongezewa, kikubwa tu asirudi nyuma na asonge mbele maana kwenye mambo ya mtandao historia inaonyesha mkali huyu ni mzuri kwa kuanzisha lakini baadaye hupotelea kusikojulikana.

 

Kwa kumbukumbu, aliwahi kuanzisha mtandao uitwao this is Diamond, akaupotezea akaanzisha mwingine Forever Diamond, akaupotezea na mtandao mwingine ni ule ambao mwisho kuposti ni Agost mwaka jana alipokuwa kwenye ‘tour’ ya Wimbo wa Salome uitwao Diamond Platnumz ambao nao anaonekana kupotezewa.

 

 

Comments are closed.