The House of Favourite Newspapers

WASAFI FESTIVAL KUKIWASHA UPYA IRINGA

BAADA ya uzinduzi wa kutisha wa Wasafi Festival kufanyika katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, mratibu wa wasanii wa tamasha hilo, Ricardo Momo amesema kuwa Ijumaa ijayo ya Novemba 30 moto unaenda kuwaka katika Uwanja wa Samora mjini Iringa.  

 

Akizungumza na Amani, Momo alisema baada ya uzinduzi huo nguvu kubwa inahamia Iringa kwenye Uwanja wa Samora ambapo wasanii wengine wapya kama Linah, Belle 9 na Afande Sele wameongezeka kwa ajili ya kunogesha burudani hizo huku wasanii wote wanaunda Lebo ya WCB watatumbuiza live.

 

“Lakini pia Novemba 30 pale Iringa kuna baadhi ya wasanii hawatakuwepo ambao ni Kisamaki, Ibra Nation, Katrina na Navy Kenzo, tunaenda sasa kuanza safari ya makamuzi yetu ikiwa ni siku kadhaa tu baada ya kuzindua Wasafi Festival yetu pale Mtwara, naomba mashabiki wote wa burudani waje kuona ni namna gani wasanii wetu wamejipanga.

 

Wasanii kwa Ujumla watakaokinukisha Iringa ukiachilia waliotajwa hapo juu ni One Incredible, Stereo na Nikki Mbishi hawa kwa upande wa Hip Hop, wengine ni Khadija Kopa, Chin Bees, Moko, Young Killer, Dudu Baya au Konki Master.

 

“Baada ya Iringa, mapinduzi ya burudani yataendelea tena kutokea siku ya Jumapili ya Desemba 2, mwaka huu ambapo tutakuwa tukiumiza nyasi za Uwanja wa Jamhuri pale mkoani Morogoro, kwani pale pia tunatarajia kuongeza wasanii huku tukipunguza ambao watakuwa na siku chache tu wametumbuiza pale,” alisema Momo.

 

Watakaongezeka kwa Morogoro ni Linah, Afande Sele, Belle 9 na Navy Kenzo lakini kwa upande wa Bongo Movie watakuwepo Aunt Ezekiel, Jacqueline Wolper na Steve Nyerere.

Stori: Musa Mateja, Amani

Comments are closed.