WASAFI FESTIVAL: RAYVANNY ATAMANI KUPAFOMU MWANZA

Rayvanny

IKIWA imebaki siku moja kuelekea siku ya Uzinduzi wa Wasafi Festival itakayofanyika Mtwara katika Uwanja wa Nagwanda Sijaona wikiendi hii, Mkali wa Muziki kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ amefunguka kutamani kupafomu wimbo wake wa Mwanza (Nyegezi) ambao umefungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kwa madai ya kukosa maadili.

 

Akizungumza na Ijumaa, Rayvanny alisema angetamani sana kwa mara ya kwanza apafomu Wimbo wa Mwanza katika jukwaa la Wasafi Festival lakini anashindwa kutokana na adhabu ya Basata ya kuufungia wimbo huo ambao yeye anakiri kuwa hakuutunga kwa nia ya kupotosha watu bali kuburudisha.

 

“Kiukweli natamani sana wangeniruhusu tu japo nipafomu katika shoo zangu maana mapokezi ya huu wimbo ni makubwa mno mpaka yananifanya nitamani kuupafomu katika jukwaa la Wasafi Festival Jumamosi hii,” alisema Rayvanny.

 

Shoo hiyo ambayo ambayo inatarajiwa kufanyika Jumamosi ya Novemba 24, mwaka huu itahusisha wakali wengine kama Country Boy, Moni Centrozone, Navy Kenzo, Khadija Kopa, Nikki Mbishi, Young Killer na wengine kibao. Lakini pia ikihusisha warembo kutoka Bongo ambao ni Lynn, Kim Nana, Aunt Ezekiel na Jackline Wolper.

Stori: Shamuma Awadhi

Toa comment