The House of Favourite Newspapers

Wasanii Bongo Kuanza Kulipwa Kutoka Nje ya Nchi

0

COSOTA (1) Mkurugenzi Mkuu wa CMEA, Paul Matthysse ‘P-Funk’ akizungumza jambo na waandishi wa habari (hawapo pichani).
COSOTA (2)Waandishi wa habari, wasanii na wadau wa sanaa nchini wakifuatilia semina hiyo.
COSOTA (4)Afisa Mtendaji Mkuu kutoka COSOTA  Bi. Doreen Sinare akiwafafanulia jambo wadau wa sanaa.
COSOTA (5)Staa wa Hip Hop, Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’ akiwa na Prodyuza Lamar wakifuatilia semina hiyo.
COSOTA (7)Staa wa Bongo Fleva, Barnabas Elias ‘Barnaba’ akiuliza swali kwa wahusika ambao ni COSOTA na CMEA.
COSOTA (8)Wadau wa sanaa wakifuatilia semina hiyo.
COSOTA (9)Mkurugenzi wa Bendi ya Stars, Aneth Kushaba akifuatilia semina hiyo.

 

GUD newz ikufikie kwako, prodyuza, meneja, msanii ama mdau wa sanaa kuwa kampuni ya kusimamia haki za muziki Copyright Management East Africa (CMEA) kwa kushirikiana na COSOTA wameshakubaliana na nchi zaidi ya tano Afrika zikiwemo Nigeria, Ghana, Afrika Kusini kuwa kazi zozote za msanii kutoka nchini Tanzania zitakuwa zikilipwa.

 

Akizungumza katika semina ya ufuatiliaji wa kazi za sanaa na Ugawaji Mirabaha kwa wasanii iliyofanyika katika Jengo la LAPF, Kijitonyama jijini Dar, Afisa Mtendaji Mkuu kutoka COSOTA  Bi. Doreen Sinare alisema kuwa tayari wameshafanya makubalino na kuanzia mwakani wasanii wataanza kulipwa.

“Tutakuwa tunatumia mtindo wa Lock Sheet ambapo sisi kama COSOTA tutakuwa tunajulishana na nchi nyingine Afrika tulizoingianazo mkataba endapo zitacheza kazi zetu watakuwa wakitutumia majina ya wasanii hao na sisi tutakuwa tukiwatumia majina ya wasanii wa kwao ambao kazi zao zimechezwa redioni.

“Ipo sheria ambayo ilishawekwa kwa TV na redio za ndani ya nchi kutumia asilimia 60 kuonesha ama kucheza kazi za ndani na asilimia 40 kwa nchi za nje,” alisema  Bi. Sinare.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa CMEA, Paul Matthysse ‘P-Funk’ alisema kuwa wameshafanya majumuisho ya redio na TV Tanzania nzima na kutakuwa na mchanganuo wa kila nyimbo, bendi, msanii kuangaliwa kazi zake zimechezwa mara ngapi.

“Tunaamini kwa mfumo huu utamjengea msanii kunufaika kwa kile anachokifanya. Kutakuwa na code itakayomuwezesha msanii kujua kazi zake zimechezwa mara ngapi kwa siku,” alisema P-Funk.

Imeandaliwa na Andrew Carlos/GPL

Leave A Reply