IRENE UWOYA, STEVE NYERERE WAITWA BASATA


BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata) limewataka wasanii wa filamu Bongo, Irene Uwoya na Steve Nyerere,  kufika katika ofisi za baraza hilo  kesho, Julai 17, 2019,  kufuatia kitendo chao cha kuwarushia fedha waandishi wa habari wakati wa kikao jana Julai 15.

Hata hivyo, Uwoya amewaomba radhi waandishi kufuatia kitendo hicho kilichosababisha baadhi ya waandishi kuharibu baadhi ya vifaa vyao kutokana na vurugu zilizotokea wakati wa kudaka fedha hizo alizokuwa anarusha

Amesema hakufanya hivyo kwa lengo la kudhalilisha waandishi wa habari kama ambavyo imetafsiriwa na watu wengi, kwani dhahiri anatambua umuhimu mkubwa wa waandishi wa habari katika jamii.

Toa comment