The House of Favourite Newspapers

Wasanii na Swaga za Kiswanglish Kwenye ‘Interview’

0

Na Ally Katalambula|IJUMAA WEKIENDA|GPL

April 17 mwaka huu Msanii wa Bongo Fleva anayechipukia kwa kasi kwenye sayari ya muziki wa Bongo ‘Hermorapa’ alitoa kali ya mwaka katika mahojiano mubashara aliyokuwa akifanya na kituo kimoja cha Tv Katika kipindi hicho mtazamaji mmoja alimuuliza Hermorapa kuwa yeye ni mtu wa aina gani jibu la msanii huyo ndio liliacha watu midomo wazi “ I’m Strong Woman” (mimi ni Mwanamke imara)

Bwana mdogo huyo alitoa jibu la namna hiyo si kwa ajili ya kufurahisha watu, bali mantiki ya kauli yake ilikuwa ni kusema yeye ni mwanaume imara, lakini kwa kutokujua vizuri Lugha ya kingeleza akajikuta anazua kioja kilicho acha gumzo.

Hili la Harmorapa limenifanya nikumbuke vioja vingine kama hivyo kutoka kwa wasanii wengine nchini, wasanii ambao kiuhalisia hawafahamu kuizungumza vizuri Lugha ya Kingereza, lakini wakiwa kwenye ‘interview’ wanachomeka maneno ya Kimombo kama swaga na bila kutarajia hujikuta wakikosea maneno hayo nakuacha gumzo kila kona.

Wasanii hao ni kama vile Shilole na maneno kama ‘Ilove is my Country, Baba Levo na maneno kama ‘This girl is my Husband’ na wengine kibao.

Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi katika hilo, kwanini baadhi ya wasanii wanapenda kuchomeka maneno ya Kingereza kwenye ‘Interview’ ilihali wakitambua Lugha hiyo ni tatizo kwao? Je Kiswahili hakitoshi kujieleza. Au ukiwa msanii usipo chomeka Kimombo kwenye ‘interview’ huonekani mjanja?.

Hata hivyo, nilichokibaini ni ulimbukeni tu wa kutokuelewa mambo sawasawa, na hili linatokana na jamii yetu kuwa na mtanzamo hasi kifikra, baadhi ya watu wanaamini kwamba mtu yeyote anayezungumza Lugha ya Kingereza ni mtu mwenye elimu kubwa na ameelimika.

Katika mtazamo huo ndipo unapokuta baadhi ya watu walioelimika na hata ambao hawajaelimika, wamekuwa wakipenda kuonekana kama wasomi katika jamii zao. Hapo ndipo balaa la kiswanglish linapo leta utata.

Utafiti uliofanywa na Gazeti la Ijumaa umebaini kuwa, wasanii hasa wa Muziki wa Bongo Fleva ndio wamekuwa wakiongoza kuchomeka maneno ya Kingereza kwenye ‘interview’ ambazo zinafanywa kwa Lugha ya Kiswahili katika vyomba mbalimbali vya habari

Sisemi watu wasizungumze wala wasijue Kingereza, ninachotaka kushauri hapa. Ni vema wasanii wakaifahamu vizuri Lugha ya Kingereza na hata Lugha za Mataifa mengine kabla ya kuitumia katika vyombo vya habari wakiwa hawaijui vizuri.

Katika ya binadamu, Ujinga si jambo baya ingawa linaweza kuwa jambo baya kama mtu ataendelea kuishi katika ujinga huo bila kujielemisha, wasanii wa Tazania wanazo sababu zaidi ya miamoja za kuifahamu Lugha ya Kingereza, hii ni kwa ajili ya mustakabali wa afya ya muziki wao.

Mwisho niwashauri wasanii wote wenye ndoto na muziki wa kimataifa, hawanabudi kujifunza kuzungumza Lugha ya Kingereza kwa mustakabari wa afya ya sanaa zao kimataifa.

Leave A Reply