Wasanii wa Kenya, Bongo ni Love + Biznesi!
HISTORIA inaonesha kuwa, msanii wa muziki wa Bongo Fleva Ambwene Yesaya ‘AY’ aliwahi kujipatia umaarufu mkubwa sana Kenya pale alipodaiwa kuwa anatoka kimapenzi na mwanadada kutoka Kenya, Cecilia Wairimu ‘Amani’.
Wawili hao licha ya kutajwa kwamba walikuwa wapenzi lakini walikuwa wakishirikiana kwenye muziki na hakika walijikuta wakifanya vizuri kibiashara Afrika Mashariki kutokana na muunganiko wao.
Hata hivyo, penzi la wawili hao ni kama lilikuwa limetawaliwa na usiri mkubwa kwa kuwa, AY alikuwa mgumu sana kuuanika na kuna wakati ikasemekana walitaka hadi kufunga ndoa lakini mambo yakaishia hewani.
Ukiachana na kapo ya AY na Amani, siku za hivi karibuni tumeshuhudia wimbi la wasanii wa Bongo wakijiweka kimapenzi kwa wale wa Kenya. Mpaka sasa dada zetu wa Bongo wawili, Amber Lulu na Lulu Diva wameshatajwa kuwadatisha wasanii wa Kenya.
Amber Lulu ambaye jina lake alilopewa na wazazi wake ni Lulu Augen aliwahi kujinasibu kujiweka kimapenzi kwa msanii mkubwa Kenya, Jackson Makini ‘Prezzo’.
Kuna wakati mwanadada huyu alilazimika kufunguka kuwa penzi analopata kutoka kwa Prezzo hajawahi kulipata kwa mwanaume yoyote Bongo kiasi kwamba anahisi sasa ametua kwa mtu sahihi.
“Kwa kweli nilipokuwa na Prezzo kunako sita kwa sita niliinjoi sana tofauti kabisa na wanaume wengine,” alisema Amber Lulu alipokuwa akiongea na paparazi wetu siku za hivi karibuni.
Haikufahamika penzi lao liliyeyukayeyukaje lakini mpaka wanatengana kila mmoja alifurahia penzi la mwenzake na hakika hata kimuziki walipaa kwa kuwa,
Amber alijulikana Kenya zaidi na Prezzo naye akazidi kujipatia jina Tanzania.
Mwisho wa siku tunaweza kuhitimisha kwamba wote penzi lao limewanufaisha kimuziki. Achana na Amber Lulu, wajina wa msanii huyo Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ naye juzikati alitrendi sana kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana akiwa kimalovee zaidi na mwanamuziki ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Starehe nchini Kenya, Charles Njagua Kanyi ‘Jaguar’.
Mwanadada huyo mbali na picha hizo kusambaa, alitamba kuwa wenye wivu wajinyonge kwani naye amepata nafasi ya kutuliza moyo wake kwa mwanamuziki huyo.
Wawili hao walikwenda zao Dubai kula bata na wapo waliosema ni kiki ila wengine wakasema ni muendelezo wa wasanii wa Kenya kujibu mapigo baada ya kuona dada zao wanachukuliwa sana na wasanii wa Bongo.
Soma mahojiano yetu na Lulu Diva akiwa Dubai hapa chini: Paparazi: Umesema upo Dubai unakula bata na Jaguar, mbona uhusiano huu kama umekuja ghafla sana?
Lulu Diva: Wala siyo ghafla kama watu wanavyodhani. Tulianza kama miezi minne nyuma na sasa tumeamua kuweka wazi.
Paparazi: Kwa hiyo Dubai mnafanya nini?
Lulu Diva: Ni kula bata tu, baadaye tutakwenda zetu Nairobi nyumbani kwa wakwe. Yote kwa yote sasa hivi Lulu Diva na Jaguar wamekuwa midomoni mwa watu wa Kenya na Tanzania ambapo hilo linaweza kuwafanya wakashaini zaidi kimuziki.
Kwa upande mwingine pia wanaweza kuendelea ‘kumegana kisela’ licha ya maelezo kwamba Bongo kuna mrembo ambaye amezaa na Prezzo.
Mbali na hao, sasa hivi penzi la msanii wa Bongo Fleva, Benard Michael Paul Mnyang’anga ‘Ben Pol’ na mwanadada kutoka Kenya, Anerlisa Muigai ndiyo limepamba moto huku mipango ya ndoa ikiendelea.
Wawili hao wamekuwa gumzo kutokana na bata wanalokula na kibiashara sasa hivi Ben Pol yuko juu.
Akitoa ngoma yake lazima ‘itahiti’ Kenya na Tanzania, hiyo ni kuonesha kuwa penzi lao linawanufaisha kibiashara pia.
Bila kumsahau msanii wa muziki Bongo, Ali Salehe Kiba ‘Alikiba’ ambaye ameamua kuoa kabisa nchini Kenya ambapo alifunga ndoa na mwanadada aitwaye Amina Rikesh.
Uamuzi wake huo umemfanya akiwa Dar ni nyumbani na akienda Kenya ni ukweni hivyo anapata sapoti kubwa kutoka kwa mashemeji zake. Funga kazi ni penzi la mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz.
MAKALA NA AMRAN KAIMA, UWAZI
Comments are closed.