The House of Favourite Newspapers

Wasanii wa Nigeria Watamba Katika Tuzo za Afrima kwenye ukumbi wa Dakar Arena Senegal

0
Muthaka kutoka Kenya akimpokea msanii bora wa kike kutoka Afrika Mashariki katika Tuzo za Muziki za Afrima, All Africa Music kwenye ukumbi wa Dakar Arena huko Diamniadio, Senegal.

Mastaa wa Nigeria kama vile Burna Boy, Davido na Wizkid wametawala katika orodha ya washindi kwenye tuzo za nane za All Africa Music Awards (Afrima).

Tala ya msanii wa Ivory Coast Didi B, ulitajwa kuwa wimbo bora wa mwaka katika sherehe ya kifahari iliyofanyika katika mji mkuu wa Senegal, Dakar.

Mwaka huu mastaa wakubwa wakiwemo rapper wa Ghana Black Sherif na wasanii wawili wa Nigeria P-Squared walitumbuiza.

Mwimbaji wa Nigeria Asake alitangazwa kuwa Mwanamuziki mpya Bora wa Mwaka.

Wakati wa hotuba yake ya kupokea tuzo Asake, ambaye jina lake halisi ni Ahmed Ololade, alisema kushinda ilikuwa ni ndoto yake kutimia Ilianza kama ndoto lakini leo ni ukweli. Shukran kwa Mungu, lebo yangu na mashabiki wangu wote wanaosikiliza nyimbo zangu.

Muziki wa Asake ulitawala ulingo wa muziki wa Afrobeats mwaka 2022 kwa nyimbo maarufu kama vile Sungba, Peace Be Unto You na Omo Ope miongoni mwa nyimbo zingine.

Muziki wake unajulikana kwa maneno ya kuvutia ya Kiyoruba na Pidgin English, mpigo unaotambulika na kauli mbiu yake – Ololade mi Asake – ambayo wasikilizaji wanaweza kusikia mwanzoni mwa nyimbo zake kadhaa.

Walakini, msanii huyo alikumbana na janga Desemba ya 2022 wakati watu wawili walifariki dunia kwenye tamasha lake huko London baada ya ajali kwenye ukumbi huo.

Burna Boy, ambaye alishinda tuzo ya Msanii Bora wa Mwaka na Albamu Bora ya Mwaka, Davido, aliyeshinda Msanii Bora wa Kiume katika Muziki wa Inspirational Afrika, na Wizkid, aliyeshinda tuzo ya Muziki bora wa Afrika magharibi hawakuwapo kwenye hafla hiyo ya kupokea tuzo zao.

Kulikuwa na utata katika kuelekea maandalizi ya tuzo hizo, baada ya watu kutia saini ombi la kumtaka mwimbaji wa Nigeria Brymo asishinde Mtunzi Bora wa Mwaka, baada ya kutuma mfululizo wa tweets za matusi kuhusu kabila la Igbo la Nigeria.

Zaidi ya watu 40,000 walitia saini ombi hilo dhidi ya mwimbaji huyo, ambaye jina lake halisi ni Olawale Ashimi. Mwishowe Iba One kutoka Mali alishinda, na Brymo ameomba msamaha, akisema hakukusudia kutoa matusi.

Senegal iliweka historia mwaka huu kwa kuwa nchi ya kwanza barani Afrika inayozungumza lugha ya Kifaransa kuwa mwenyeji wa tuzo hizo ambazo zina ushirikiano na Umoja wa Afrika.

UTAPENDA NANDY ALIVYOMTAMBULISHA MSANII WAKE YAMMI, AFUNGUKA – “BILLNASS ANAUMWA”…

Leave A Reply