The House of Favourite Newspapers

Wasanii Waahidi Makubwa Mbele Ya Rais Magufuli

Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dkt. Kiagho Kilonzo akizungumza kwenye mkutano huo.

Bodi ya Filamu nchini leo imewaongoza wasanii wa muziki na maigizo na wengineo katika kikao cha mwisho cha maandalizi ya tamasha la kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere litakalofanyika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere uliopo Posta jijini Dar

 

Katika mkutano huo ambao mgeni rasmi atakuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli wasanii mbalimbali wameahidi kushiriki na kutoa burudani.

Rais wa Shirikisho la muziki nchini, Ado Novemba (kushoto) akieleza jinsi wanamuziki watakavyoshiriki tamasha hilo.

Rais Magufuli anatarajiwa kupewa tuzo na wasanii hao kutokana na umahiri wake wa kazi unaoendana utendaji wa Hayati Baba wa Taifa. Katika kuhitimisha tamasha hilo wasanii hao watakwenda kutoa burudani ya bure kwenye viwanja wa Zakhem vilivyopo Mbagala Dar.

MwanaFA naye akithibitisha kufanya yake kwenye tamasha hilo.
AT naye akithitisha kuwemo ndani ya nyumba.
Mkutano ukiendelea.
Msanii wa Bongo muvi, Halima Yahaya ‘Davina’ amesema yeye na wenzake nao watanogesha tamasha hilo.
Mkali ngonjera, Mrisho Mpoto a.k.a Mjomba akiahidi kufanya balaa kwenye tamasha hilo.

HABARI:NEEMA ADRIAN | PICHA: RICHARD BUKOS

Comments are closed.