Wasanii Waaswa Kusajili Kazi Zao na Majina yao ya Kisanii
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Suleimani Jafo, atoa wito kwa Wasanii kusajili majina yao ya kisanii BRELA kama alama ya biashara na kazi zao COSOTA kwa ajili ya kuweka ulinzi.
Mheshimiwa Waziri Dkt.Jaffo ametoa wito alipokuwa akifungua mkutano wa maadhimisho ya Miliki Ubunifu Duniani Kitaifa yaliyofanyika leo Mei 21, 2025 Dar es Salaam, na yana Kauli Mbiu isemayo Muziki na Miliki Bunifu: Sikiliza Mdundo wa Miliki Bunifu.”
“Napenda kuwapongeza Wasanii wote wa Muziki waliosajili majina yao BRELA akiwemo Diamond platinum, Nandy, Zuchu, Mrisho Mpoto na wengine wote, usajili huu unatoa nafasi kubwa ya kukuza kipato na kufanya biashara kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu.
“Tunasisitiza Muziki si burudani tu, ni biashara na biashara yoyote inalindwa kisheria, hivyo Wasanii wengi wamekuwa wakipoteza mapato kwa sababu kazi zao hazijasajiliwa,” alisema Nyaisa.
Maadhimisho hayo yamefanyika yameratibiwa na BRELA na kushirikiana na COSOTA.
Akiendelea kuzungumza Mheshimiwa Waziri huyo alisema hapo nyuma Wasanii wengi wamepoteza haki zao ijapokuwa wamefanya kazi kubwa kwa sababu hawakuzingatia haya.
Wasanii wa muziki nchini wametakiwa kusajili kazi zao na kuzilinda kupitia mifumo rasmi ya miliki bunifu ili kunufaika kiuchumi na kulinda kazi zao dhidi ya wizi wa ubunifu.
Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Godfrey Nyaisa amesema licha ya Muziki wa Tanzania kuvuka mipaka ya nchi, Wasanii wengi bado hawajachukua hatua ya kusajili kazi zao, jambo linalowanyima fursa ya kunufaika na kazi hizo kisheria.