WASANII WAGUSWA NA UGONJWA WA RUGE

ZIKIWA zimepita siku kadhaa tangu kaka wa Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, Mbaki aeleze hali ya afya ya mkurugenzi huyo na kuomba mchango ili aendelewe kutibiwa, baadhi ya wasanii wameonesha kuguswa na hali hiyo.  

 

Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, wasanii hao wameguswa kwa kuweka mahojiano hayo huku wengine wakitumia nafasi hiyo kuomba Watanzania na wadau wa burudani kusaidia. Wasanii na watangazaji walioguswa na kuweka video na mahojiano hayo ni Madee, Roma Mkatoliki, Nikki wa Pili, Zamaradi Mketema, Fid Q na wengine wengi.

Katika akaunti zao wameweka;“Mbaki Mutahaba, ambaye ni mdogo wa #RugeMutahaba ameeleza kwamba ni wazi kwamba gharama za matibabu ya Ruge ni kubwa mno. Amesema Rais Dkt Magufuli na wengine walichangia lakini gharama hizo ni kubwa kuliko kawaida.

“Gharama za matibabu kwa kule ni kubwa na kwa siku inaweza kufika million 5 mpaka 6, kuna number ambayo imeandikishwa kwa jina la mdogo wetu, Kemilembe Mutahaba 0752 222 210 hiyo ndiyo namba ambayo watu wanaweza kutuma sms za pole, faraja na hata wengine ambao wangetamani kutuma chochote,” Mbaki Mutahaba.

Loading...

Toa comment