Wasanii wakubwa 4 wagoma kutumbuiza kwenye tuzo za Grammy 2019

 

RAPA Drake, Kendrick Lamar, Chaldish Gambino  na mwanadada Ariana Grande, wailiipiga chini ofa ya kutumbuiza kwenye tuzo za Grammy mwaka huu 2019.

 

Kendrick Lamar anashikilia orodha ya kuongoza kwa kugombea tuzo hizo kwenye vipengele nane, akifuatiwa na Drake vipengele saba na Chaldish Gambino vipengele vitano.  Lakini wote hao wamekataa kutumbuiza siku hiyo, ila haijajulikana pia kama wataweza kwenda kwenye tamasha hilo ili kuchukua tuzo au la.

 

Mtayarishaji wa tamasha hilo, Ken Ehrlich alisema kwamba, “Jambo la kweli ni kwamba tutaendelea kupata matatizo na dunia ya muziki wa rap, wakati wanapokosa tuzo huwa wanakataa fursa zinazoandaliwa na Grammy kwa ajili yao, thamani yetu inazidi kupungua kwenye jamii ya muziki wa rap”.

 

Sababu ya muimbaji wa Pop, Ariana Grande, kukataa kutumbuiza katika tamasha hilo  ni kumlalamikia mtayarishaji wa tuzo hizo akidai kuwa alimkataza kutumbuiza wimbo wake mpya wa “7 Rings”.

 

Tuzo za 61 za Grammy zinategemewa kufanyika Jumapili Februari 8, host akiwa ni Alicia Keys na watambuizaji wakiwemo Cardi B, Travis Scott, Post Malone, Janelle Monáe, H.E.R. Camila Cabello, na Jennifer Lopez.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club


Loading...

Toa comment