The House of Favourite Newspapers

Wasanii Wanaoishi Bongo Bahati Mbaya Tu

0

 

Staa wa Bongo Fleva,Juma Jux.

Makala: Andrew Carlos| Ijumaa | Show Biz

KWA wapenda burudani kuna wakati unasikia wimbo wa msanii kutoka nje ya nchi kwa mara ya kwanza na kutamani kabisa kama mwanamuziki huyo angekuwa raia wa Bongo tena akipiga shoo nyingi kwa pesa ya madafu.

Lakini pia wapo wanamuziki ndani ya Bongo wanaofanya vizuri kwenye muziki hususan Bongo Fleva ambao kwa muziki wao ukiusikiliza unaona kabisa walistahili kuishi ‘mbele’ wakafanya muziki huko na hapa Bongo wapo tu kwa bahati mbaya.

Katika makala haya yanawachambua baadhi tu ya wakali ambao kimuziki na kimuonekano wao wanaonekana kustahili kuwa mbele;

Staa wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’.


Vee Money

Ni msanii wa kike pekee Bongo aliyeweza kupenya kimataifa zaidi. Ameshafanya ngoma kibao na wakali wa nje ya nchi kama Orezi, Ice Prince na Reekado kutoka Nigeria pia kolabo nyingine hazijatoka ikiwemo ya Trey Songz wa Marekani.

Staa wa Bongo Fleva, Young D.

Young D

Kimuonekano, staili anayotumia katika nyimbo zake ni wazi ukimsikia ni kama anaishi Bongo bahati mbaya. Ndiyo kwanza ameanza kubamba nje ya Afrika Mashariki lakini naye anastahili kufanya muziki mbele.

Mwanamuziki wa kike wa Hip Hop Bongo, Tammy.

Tammy

Anaingia katika listi hii kuwa miongoni mwa wakali wa kike wa Hip Hop Bongo wanaofanya vizuri ambapo ukimsikia utatamani afanye muziki mbele. Staili yake ya kuchana inamuweka kufanana na wakali kutoka Marekani, Iggy Azalea na Nicki Minaj.

Staa wa Hip Hop Bongo, Ibrahim Ayoub Mandingo ‘Country Boy’.

Country Boy

Mwenyewe hupenda kujiita Shaba, jina la mkongwe wa Muziki wa Dancehall kutoka Jamaica. Muonekano wake na staili yake ya kuchana kwa muda mrefu bila kupumzika umemfanya kuingia katika listi ya wakali ambao wanastahili kupiga muziki mbele.

 

Staa wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’.

Dogo Janja

Alivyoanza muziki alionekana kama hataweza kukabiliana na gemu kutokana na udogo wake. Lakini kwa sasa ukimsikiliza nyimbo zake tatu za mwisho, My Life, Kidebe na Unavaaje Upendeze utagundua kuwa anaishi Bongo bahati mbaya.

Wildad

Mmoja wa memba kutoka Lebo ya The Industry akiwa sambamba na Rosa Ree. Wapo wanaomuona kama Chris Brown wa Bongo kutokana na muonekano na staili anayoimba. Ukimsikiliza kwenye Ngoma ya Feel Good akiwa na mabosi wake, Navy Kenzo au ngoma yake ya Get It On ni wazi utasema anaishi bongo bahati mbaya.

Jux

Mbali na muonekano wake na staili ya muziki wa R&B anaofanya, uhusiano wake na Vee Money ulimuweka katika ramani nyingine huku wengi wakiwafananisha kama wanamuziki wa Marekani, Beyonce na Jay-Z. Amekuwa akifananishwa na mkali Trey Songz kutokana na michoro ya tatoo za maandishi kifuani na hata kubadilika badilika katika nyimbo zake.

Rosa Ree

Kama ilivyo kwa Wildad, Rosa naye ni kichwa kinachoumana na Tammy katika gemu ya Hip Hop kwa wanawake. Muonekano na staili ya kuchana kwa haraka imemuweka katika ramani nyingine. Zipo baadhi ya ngoma zake alizoachia kama vile…ambazo ukizitazama ni wazi utasema anaishi Bongo bahati mbaya.

Bill Nass

Wengi wamezoea kumuita Bill Nenga. Anaingia katika listi hii kutokana na swaga za ‘floo’ yake kufananishwa na Jay-Z, 50 Cent, Nas kwa jinsi anavyopangilia maneno. Nyimbo zake Ligi Ndogo, Chafu Pozi na Mazoea ukisikiliza
anavyotamka maneno utaamini kwa nini anaishi Bongo bahati mbaya.

Leave A Reply