Wasanii Wauaga Mwili wa Mzee Majuto Karimjee (Picha + Video)
MAMIA ya waombolezaji wamejitokeza katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kuaga mwili wa aliyekuwa muigizaji nguli wa vichekesho nchini, Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ leo Agost 9, 2018.
Mzee King Majuto alifariki dunia jana Agosti 8, 2018 majira ya saa 2:00 usiku katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu kwa siku kadhaa.
Baada ya kuaga, mwili ulisafirishwa kwenda nyumbani kwake jijini Tanga kwa maziko ambayo yatafanyika kesho Ijumaa.
Baadhi ya wasanii waliofika Wema Sepetu, Salma Jabu ‘Nisha’, Steve nyerere, Diamond Platnumz, Ray, Shamsa Ford, Rich Mavoko, Rommy Jones na wengineo wengi.
(PICHA: RICHARD BUKOS | GPL)
Comments are closed.